The House of Favourite Newspapers

T-PAIN AKAMATWA NA BUNDUKI UWANJA WA NDEGE

T-Pain.

MLINZI wa rapa Mmarekani,  T-Pain, juzi alikamatwa uwanja wa ndege akiwa na begi la mkuu wake huyo ambamo ilikutwa bastola wakati wa ukaguzi kwenye uwanja wa ndege wa Atlanta, Georgia.

Hata hivyo, pamoja na polisi kutotaja jina la mlinzi huyo,  bastola hiyo aina ya Smith & Wesson .380 iliyokuwa na risasi, ilirudishwa kwa rapa huyo na yeye na mlinzi wake waliachiwa bila ya kufunguliwa mashitaka.

Pamoja na hayo, inasemekana polisi wanachunguza iwapo wamfungulie mashitaka mlinzi huyo au la.

Uwanja wa ndege wa Atlanta iliponaswa bastola.

 

Comments are closed.