The House of Favourite Newspapers

TAARIFA RASMI ZA HAJI MANARA KUTIMULIWA SIMBA HIZI HAPA…

Ofisa Habari wa timu ya Simba, Haji Manara.

Kuanzia jana jioni hadi usiku kulikuwa na taarifa inayosambaa kuwa Klabu ya Simba imeamua kumtoa kwenye nafasi ya Ofisa Habari, Haji Manara kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

 

Taarifa hizo zilienea kwa kasi na kusambaa hasa kwenye magrouup ya mitandao ya kijamii, lakini hakukuwa na tamko rasmi kutoka Simba juu ya maamuzi hayo.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara amelizungumzia hilo kwa kueleza kuwa hakuna kitu kama hicho na kuwatolea ‘povu’ wale wanamchukia na kusambaza taarifa ambazo siyo za kweli.

 

Manara ameweka picha ya mtu aliyesambaza taarifa hizo kupitia Instagram kisha akaandika maelezo haya:

“Kuna mpumb** mmoja aliyejitambulisha kama Mwenyekiti wa Group la Yanga WhatsApp supporters makao makuu, anazusha mitandaoni kuwa nimeondoka Simba…hahahahaha sitakaa milele pale kama yeye na wapumb** wenzie watavyoondoka huko walipo, lakini kwa sasa mm ndiyo msemaji wa Big brand ya nch….. , unavyozidi kunichukia ndiyo unazidi kunisogeza…. Kwa mnaoniogopa wote niwaambie NA BAO.”

Comments are closed.