The House of Favourite Newspapers

TAARIFA YA FAMILIA KUHUSU MSIBA WA MZEE KINGUNGE

Waombolezaji waliofika kumpa pole katika msiba huo.
Waombolezaji waliofika kumpa pole katika msiba huo.
Kinjekitile akitoa ufafanuzi kuhusu mazishi ya baba yake marehemu Ngombale Mwiru.
Taswira mbalimbali katika msiba huo.
Kinjekitile (kulia) akishauriana jambo na ndugu zake.

 

KINJEKITILE Ngombale Mwiru ambaye ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe nchini, marehemu Ngombale Mwiru ambaye amefariki leo asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, amesema taratibu za mazishi ya baba yao zitafanyika baada ya familia kukaa pamoja leo.

 

Akizungumza na waandishi wa habari waliofika nyumbani kwao, eneo la Victoria, Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, amewapongeza madaktari wa Hospitali ya Muhimbili kwa jitihada zao za kupigania uhai wa marehemu lakini Mwenyezi Mungu alimpenda zaidi.

 

“Baada ya baba kuumwa na mbwa alianza kupata complications (matatizo) ya moyo na mapafu, hivyo kwa muda wa siku tatu alihangaika sana wakati akipatiwa matibabu, hivyo cha msingi ni sisi kumwombea kwa Mungu apumzike kwa amani,” alisema Kinjekitile.

 

 

Comments are closed.