The House of Favourite Newspapers

DENTI AUAWA KWA UMEME AKICHAJI SIMU BAFUNI

Kseniya wakati wa uhai wake.  Msichana huyo alikutwa akiwa amezimia kabla ya kufa akiwa katika jakuzi alilokuwa akiogea huku simu yake iliyokuwa kwenye chaji, ikiwa inaelekea kwenye maji.

 

Taswira nyingine ya Kseniya wakati wa uhai wake.

MWANAFUNZI mwenye umri wa miaka 12 wa kijiji kilicho karibu na  jiji la Mosow, Russia,  aliyetajwa kwa jina  la Kseniya P., hivi karibuni amekutwa amekufa bafuni baada ya simu yake (smartphone) aliyokuwa anaichaji pembeni, kutumbukia kwenye jakuzi alimokuwa  akioga.

 

Polisi wanaamini mtoto huyo alikuwa akisikiliza muziki wakati simu hiyo ilipoishiwa chaji na kuanguka majini,  jambo lililosababisha umeme kumfikia kutoka kwenye waya uliokuwa ukitumika kuchajia chombo hicho.

 

Kseniya aliyekuwa ametoka kucheza mpira wa kikapu shuleni, alifikia bafuni kuoga, lakini mama yake aliposikia ukimya bafuni, alimfuata na kumkuta tayari  kichwa chake kikiwa majini na simu ikielea kwenye maji.

 

Mama huyo alijaribu kuokoa maisha ya binti yake, lakini Kseniya  alikuwa tayari amekufa.

 

Mtoto huyo alikuwa ndiye pekee katika familia yake inayoishi kijiji cha Bolshoe Gryzlovo, wilaya ya Serpukhovsky, mkoa wa Moscow.

 

WALUSANGA NDAKI/MITANDAO/MASHIRIKA YA HABARI

Comments are closed.