The House of Favourite Newspapers

Takukuru: Miradi 171 Yenye Thamani Ya Sh Bilioni 143.3 Ilikuwa Na Utekelezaji Hafifu

0
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), CP Salum Hamduni

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), CP Salum Hamduni leo Machi 28, 2024 amesema katika uchunguzi wa miradi 1800, miradi 171 yenye thamani ya Sh bilioni 143.3 ilikuwa na utekelezaji hafifu.

Akizungumza kabla ya kukabidhi ripoti za uchunguzi kwa Rais Samia Suluhu katika IKulu ya Chamwino leo Machi 28, CP Hamduni amesema miradi hiyo ilikuwa katika sekta ya Ujenzi, Fedha, Maji, Kilimo na Majengo.

“Tulitoa mapendekezo 3,668 ili kurekebisha kasoro zilizobainika. Jumla ya mapendekezo 2,740 yalitekelezwa,” amesema.

Leave A Reply