The House of Favourite Newspapers

Takwimu za Makambo Kwa Waarabu ni Hatarii

Heritier Makambo

ALICHOKIFANYA straika, Heritier Makambo, Yanga iliposhinda mabao 2-1 dhidi ya USM Algiers kwenye Uwanja wa Tai­fa kinaonyesha kwamba jamaa ni jembe.

 

Takwimu za kile alicho­fanya Makambo dakika 90 zinaonyesha kuwa ni mche­zaji hatari kama ataendelea kuonyesha juhudi akiwa na vijana hao wa Jangwani am­bao sasa wana mzuka wa kurejea kwa Yusuf Manji.

 

Makambo ndiye alikuwa gumzo kwa mashabiki wa timu zote za Simba na Yanga ambao walihud­huriwa kwenye mchezo huo wa kimataifa ambao Yanga ilikuwa inakamilisha ratiba tu.

 

Kabla ya mchezo huo, Makambo alikuwa ame­funga mabao matatu kwenye michezo mitatu ya kirafiki lakini aliendelea kuonyesha umahiri wake kwenye mechi hiyo baada ya kufunga bao moja kati ya mawili ya timu yake.

 

Katika dakika hizo tisini za Jumapili, Makambo ali­gusa mpira mara 24, huku akipiga pasi 18 zilizofika, al­ichezewa madhambi mara saba akiwa ndiye mchezaji aliyechezewa madhambi mara nyingi kwenye mechi hiyo iliyokuwa na mashabiki wachache.

 

Mbali na hilo, staa huyo ambaye kocha Mwinyi Zahera wa Yanga anasisi­tiza ni kifaa, alifunika tena kwenye kupiga mashuti ambapo alipiga jumla ya mashuti manne kwenye dakika zote alizocheza.

 

Mashabiki wa jukwaa la Simba wakati wa kutoka uwanjani walikuwa wakim­zungumzia na kila mmoja alisifu kuhusu uwezo wake uwanjani ambapo aliibuka staa kwenye mechi hiyo.

Comments are closed.