The House of Favourite Newspapers

Tamasha Kubwa La Pasaka Kufanyika Viwanja Vya Leaders Club Dar, Kesho

0
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akizungumza na vyombo vya habari kuelekea tamasha la pasaka linalotarajiwa kufanyika kesho Jumapili ya Pasaka.

Dar es Salaam, 8 Aprili 2023: Maandalizi ya Tamasha kubwa la Pasaka linalotarajiwa kufanyika kesho katika Viwanja vya Leaders Club vilivyopo Kinondoni jijini Dar yanaendelea ikiwa ni pamoja na maombi ya kuliombea taifa watu wote wanakaribishwa kuhudhuria.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Msama Promotion ambaye pia ni Mwandaaji waa tamasha hilo, Alex Msama amesema tamasha hilo ambalo litakwenda kupamba siku hiyo ni pamoja na kuwa na waimbaji mahiri wa nyimbo za injili.

Msama amesema katika tamasha hilo waimbaji wote wapo tayari kwa ajili  na kuongeza kuwa kutakuwa na  maombi maalum ya kumuombea Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili na kwa kufanya kazi kubwa ya kuindesha nchi.

“Mgeni rasmi tulitegemea angekuwa ni mama yetu “Dk.Samia Suluhu Hassan lakini kutokana na majukumu ya kuliongoza taifa, Waziri wetu wa Habari Nnape Nnauye atamuwakilisha na kutakuwa na maombi ya kumshukuru Mungu kwa miaka miwili ambayo Rais wetu ametuongoza vyema.

“Pia kutakuwa na michezo ya watoto kama vile, kubembea, kuseleleka na mingine mingi, naendelea kusisitiza kuwa hakuna kiingilio itakuwa ni bure na usalama wa hali ya juu kwa watu na mali zao na kuwaomba wananchi kuja kufurika kwenye tamasha hilo ili wajionee burudani hiyo itakayoacha gumzo” amesema Msama.

Katika  tamasha hilo miongoni mwa wasanii wa nyimbo za injili watakaokuwepo ni Masi Masilia kutoka Congo DRC, Faustine Munishi kutoka Kenya, Tumaini Akilimali kutoka Kenya Joshua Ngoma kutoka Rwanda, Nicole Ngabo kutoka Congo, Upendo Nkone, Abwene Mwasongwe na wengine kuto andani na nje ya nchi.

Leave A Reply