The House of Favourite Newspapers

TAMASHA KUBWA LA SPEAKERS CONFERENCE KUTIKISA DAR KESHO

TAMASHA kubwa lenye jina la Speakers Conference linatarajia kuunguruma kesho katika Ukumbi wa Ubongo Plaza jijini Dar.

Mmoja wa wasemaji wa tamasha hilo lililoandaliwa na Kampuni ya Road to Success, Mohamed Ngoma amewataka vijana kujitokeza kwa wingi kuweza kupata elimu ya kijasiriamali na maisha kwa ujumla.

Alisema kutakuwepo na wazungumzaji mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa Global Group, Eric Shigongo, Antony Luvanda, Chris Mauki, Haris Kapiga na mzungumzaji kutoka Botswana, Ludzi Mazwiduma.

“Hii si ya kukosa, watu wafike kwa wingi kwa kiingilio cha shilingi 30,000, 50,000 na laki moja kwa VIP,” alisema Mohamed.

 

Naye Ludzi amesema, hii nafasi ya pekee kwa Watanzania kupata chakula cha ubongo hivyo kuwaomba wajitokeze kwa wingi ili waweze kujifunza mbinu mbalimbali za kufanikiwa maishani pamoja na masuala ya biashara.

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwatafuta waratibu kwa namba zao za simu; 0674 502925 au 0654 864847.

Stori: Mwandishi Wetu

Comments are closed.