The House of Favourite Newspapers

Tamasha Kubwa La Vijana Kulindima Tena

Mkurugenzi wa Global Group, Eric Shigongo (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana na maandalizi ya tamasha hilo. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Mchungaji Dkt. Huruma Nkone na Samuel Sasali ambaye ni mwanakamati.

Wanachuo na vijana kutoka pande mbalimbali za jiji la Dar Novemba 15 mwaka huu wanatarajiwa kupata burudani kukusanyika kwenye mkesha wa tamasha kubwa na kiroho lililoandaliwa na Kanisa la Kanisa la TAG–Victory Christian Centre Tabernacle kwa kushirikiana na Jumuiya za Kikristo na Serikali za wanafunzi wa vyuo.

Akizungumza na wanahabari leo kwenye kanisa hilo lililopo Kawe Beach jijini Dar Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Mchungaji Dkt. Huruma Nkone amesema linatarajiwa kufanyika viwanja vya Tanganyika Packers jijini.

Mkutano ukiendelea.

Mchungaji Nkone amesema tamasha hilo ambalo limekuwa likitumika kuwapa moyo na kuwajenga kiroho vijana hao limeshafanyika mara nane kwa mafanikio makubwa na safari hii limeongezewa nguvu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye amekuwa mmoja wa waandaaji.

Dkt. Nkone ambaye atakuwa mshasishaji wa kuwajenga kiroho na kiakili vijana hao amewataja wazungumzaji wengine kuwa ni Mkurugenzi wa Global Group, Eric Shigongo, Samuel Sasali. Dkt. Hellen Gwambaye na Salome Msimbe.

Mchungaji Dkt. Nkone akizungumza kwenye mkutano huo.

Dkt. Nkone amesema amehakikishiwa na Makonda uwepo wa usalama wa kutosha kwa watakaohudhuria tamasha hilo wao pamoja na mali zao.

Tamasha hilo pamoja nakuwajenga kiuzalendo vijana hao litambambwa na burudani kutoka makundi mbalimbali ikiwemo, Zabron Singers, Upendo Nkone, Joel Lwaga, Walter Chilambo, Students Mass Choir, Beda Smith, Hype Squad Dancers na Rivers of Joy International.

Baada ya kuzungumza hayo Shigongo alisema tamasha hilo lina msingi mkubwa sana wa kuwajenga kiroho vijana hao na kusema usipowajenga vyema vijana si rahisi kupata taifa bora.

Shigongo akisistiza jambo.

“Vijana wanatakiwa kupewa hamasa na kujengwa kiroho ili waweze kufikia malengo yao.

Tukiwa na taifa lenye watu wenye hofu ya mungu ni lazima tupige hatua kubwa ya kimaendeleo.

Tatizo kubwa lililopo hapa nchini kwa sasa ni vitu kama kukosa uaminifu hivyo kutoaminiwa jambo ambalo linawafelisha wengine kwenye koneksheni za mafanikio” Alisema Shigongo na kuwataja vijana kufika kwa wingi kwenye tamasha hilo ambalo kiingilio ni bure.

Comments are closed.