The House of Favourite Newspapers

Tamasha la Kili Dome Kufanyika Kwa siku tatu Mfululizo Mkoani Kilimanjaro

0
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Irene Mutiganzi akisungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) mjini moshi katika Garden ya Hugo’s wakati wa kutangaza tamasha la Kili Dome linalotarajiwa kufanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo Hogo’s Moshi Kilimanjaro kuelekea kilele cha Mbio za Kili Marathoni zinazotarajiwa kufanuyika Machi Mosi 2020 Mkoani humo.

 

Moshi, Februari 26, 2020: Tamasha maalumu kuelekea kilele cha mbio za Kili Marathon 2020, maarufu kama Kili Dome linatarajiwa kufanyika Ijumaa, Jumamosi na Jumapili baada yambio za Kili Marathon wiki hii mjini Moshi ikiwa ni siku tatu kuelekea kilele chambio hizo kufanyika.

Tamasha la Kili Dome litakalofanyika katika Ukumbi wa Hugo’s linalenga kuwakutanisha wadau na washiriki wote watakaoshiriki katika mbio za Kili Marathon mwaka huu zilizopangwa kufanyika Machi Mosi mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza mjini hapa, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Irene Mutiganzi alisema kuwa maandalizi kwa ajili ya Kili Dome yamekamilika rasmi.

Alisema tamasha hilo litapambwa na burudani kutoka kwa wasanii mbali mbali ikiwamo wasanii maarufu kama Marioo, Mimi Mars, Maua Sama na G.Nako ambao alisema wote kwa pamoja wamejiandaa vyema kutoa burudani safi kwa wakazi wa Moshi, maeneo ya jirani pamoja na watu wote waliosafiri kwa umbali mrefu kuja kushiriki kilele cha mbio za Kili Marathon 2020.

“Kwenye Kili Dome ndipo tunapokutana wadau wote ikiwa ni siku tatu kabla ya kuelekea katika kilele cha mbio za Kili Marathon Jumapili hii. Tunawakaribisha wa wakazi wote wa Moshi na wageni waliyokuja kwenye mbio hizi kwenye Kili Dome ya mwaka huu.” alisema Mutiganzi. Kama wadhamini wakuu wa Kili Marathon, Bia ya Kilimanjaro Premium Lager mwaka huu imejiachie kivingine kabisa na Kili Canvas ili kutoa hamasa kwa wakimbiaji wote.

Kili Canvas ambayo kwa sasa ipo Key’s Hotel hapa Moshi ina teknolojia ya kisasa ambapo mkimbiaji akipita karibu yake anapigwa picha kwa utaalam uliobuniwa na picha hiyo inatumwa kwenye simu ya mkimbiaji huyo kwa wakati huo huo. Mkimbiaji anapaswa kujisajili kwanza na kupatiwa Chip maalum.

Kabla ya kuletwa hapa Moshi, Kili Canvas ilikuwa katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam, ambapo wakimbiaji mbalimbali walipata fursa ya kuishuhudia.

Leave A Reply