The House of Favourite Newspapers

Tamasha la Majimaji Selebuka 2015 lafana

0

Kikundi cha Jakaya Sanaa kilichoibuka bingwa wa shindano la Ngoma za Asili kwenye Tamasha la Majimaji Selebuka 2015 yanayoendelea kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa ya Vita vya Majimaji, Songea.

Kikundi cha Ngoma cha Lihanje-Ngoma ya Mganda wakifanya yao katika Shindano la Ngoma za Asili kwenye tamasha la Majimaji Selebuka 2015.Jaji Mkuu katika Shindano la Ngoma za Asili, Balthazar Namusya akimvisha Medali ya Shaba mkuu wa Kikundi cha Ngoma cha Lihanje Ngoma ya Kioda kilichoshika nafasi ya tatu kwenye Tamasha la Majimaji Selebuka.

Mmoja wa Wanakikundi cha Jakaya Sanaa, akipokea zawadi ya fedha taslim, medali ya dhahabu na cheti kama bingwa wa shindano la Ngoma za Asili katika Tamasha la Majimaji Selebuka 2015 linaoendelea kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji, Songea.

Majaji wa Ngoma za Asili wakiwa na vyeti vyao walivyotunukiwa katika Tamasha la Majimaji Selebuka 2015, linaloendelea kwenye Uwanja wa Makumbusho wa Mashujaa wa Vita vya Majimaji mjini Songea. Tamasha hilo limeratibiwa na Asasi ya Somi.

Mkurungenzi mwenza wa Asasi ya Somi, Dk Damas Ndumbaro wa pili kutoka kushoto akifuatilia kwa ukaribu Shindano la ngoma za asili katika tamasha la kila mwaka la Majimaji Selebuka 2015 kwenye Uwanja wa Makumbusho wa Mashujaa wa Vita vya Majimaji, Songea.

Wasanii kutoka vikundi vitatu tofauti vilivyofanikiwa kuingia fainali ya shindano la Ngoma za Asili katika tamasha la majimaji selebuka wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutunukiwa zawadi zao. Tamasha hilo linaendelea kwenye Uwanja wa Makumbusho wa Mashujaa wa Vita vya Majimaji, Songea.

 

Leave A Reply