The House of Favourite Newspapers

Tambwe: Lazima niifunge APR

0

AMISSI TAMBWE-001

Straika wa Yanga, Amissi Tambwe.

HUKU akionyesha kujiamini, straika wa Yanga, Amissi Tambwe, amekula kiapo cha kucheza kwa kujituma na kuifunga APR katika mchezo wa leo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Amahoro jijini hapa.

Tambwe ambaye anaunda safu kali ya ushambuliaji ya Yanga ya MTN akiwa na Simon Msuva na Donald Ngoma, amejizolea umaarufu jijini hapa na mashabiki wengi walijitokeza kumuona mazoezini juzi kwenye viwanja vya Shirikisho la Soka Rwanda (Ferwafa).

Yanga na APR zinakutana kwenye mchezo wa kwanza raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufanya vizuri kwenye mechi za awali.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Tambwe alisema licha ya kutowajua vizuri APR, anaamini hilo haliwezi kumzuia kufunga katika mchezo huo.

“Nawaheshimu wapinzani wetu, siwajui vizuri lakini kwa jinsi tulivyojiandaa, hawawezi kutupa ugumu uwanjani, mashabiki wetu wasiwe na wasiwasi.

“Nimejipanga vizuri kwa mchezo huo, unajua kilichonileta hapa ni kuisaidia Yanga ipate ushindi, nitahakikisha nafunga hata bao moja,” alisema Tambwe, mwenye mabao 17 katika Ligi Kuu Bara.

Tambwe ana bao moja katika Ligi ya Mabingwa Afrika, sawa na Thabani Kamusoko na Ngoma. Katika kikosi cha APR, Abdul Rwatubyaye ana mabao matatu kwenye michuano hiyo.

Leave A Reply