The House of Favourite Newspapers

Tamisemi Yazindua Mkoba Wa Siku 1000

tamisemi-1

Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Dk. Zainab Chaula akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi huo.

tamisemi-2

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Joyceline Kaganda akimkabidhi mikoba hiyo kwa ajili ya uzinduzi.

tamisemi-3

Baadhi ya wageni waalikwa waliofika katika hafla hiyo.

tamisemi-4

Hafla hiyo ikiendelea.

tamisemi-5

…. Dk. Chaula akizungumza jambo katika hafla hiyo.

NAIBU Katibu Mkuu TAMISEMI, Dk. Zainab Chaula amezindua mradi wa lishe wa mwanzo bora wenye lengo la kuboresha lishe ya akina mama na mtoto ambao  umepewa jina la ‘Mkoba wa Siku 1000’.

Akizungumza jana katika hafla hiyo,Dk. Chaula alisema kuwa, uzinduzi wa mkoba huo unalengo la kupunguza kwa asilimia 20 udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka miwili na pia upungufu wa damu kwa akina mama wajawazito.

Mradi huo wa miaka saba unafadhiliwa na watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) ambapo jana ulizinduliwa rasmi Kitaifa.

(HABARI: DENIS MTIMA/GPL)

Comments are closed.