The House of Favourite Newspapers

TAMKO la POLISI Kuhusu MAUAJI Kigoma “Tutawalaza Wote” – Video

Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Liberatus Sabas amewahakikishia wakazi wa Mkoa wa Kigoma kuimarishwa kwa usalama mkoani humo kutokana na kukithiri kwa matukio ya uhalifu wa kutumia silaha uliosababisha wananchi kuishi kwa hofu na wengine kuuhama mkoa huo.

 

Sabas ameyasema hayo kufuatia matukio ya mara kwa mara ya utekaji na uporaji kwa kutumia silaha ambapo amebainisha kuwa juhudi zaidi zinafanyika kutokomeza vitendo hivyo ambapo amesema tayari Kikosi Maalumu cha Jeshi la Polisi kinaendelea na oparesheni ya kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama mkoani Kigoma inarejea.

 

Aidha, Kamishna Sabas amesema jeshi hilo halitasita kuchukua hatua za kisheria kwa raia wa kigeni watakao bainika kuhusikaa na uhalifu huo.

VIDEO: MSIKIE SABAS AKIZUNGUMZA

Comments are closed.