The House of Favourite Newspapers

Tamwa, Wadau Wakutana Kujadili Rushwa Ya Ngono

0

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa jinsia na habari wakiwemo Wahariri, Dawati la Jinsia, wanafunzi na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), leo Jumanne, Oktoba 17, 2023 wamefanya semina ya majadiliano maalum kuhusu masuala ya rushwa ya ngono kwenye vyumba vya habari.

Majadiliano hayo ya wazi (open discussion) yalijikita katika maswali matatu makubwa ambayo ni; uelewa juu ya rushwa ya ngono, nini wanaume wanapaswa kufanya kupunguza au kuondoa rushwa ya ngono kwenye vyombo vya habari?

Na wanawake wafanye nini ili kudhibiti au kuondoa rushwa ya ngono?

Msimamo wa pamoja juu ya majadiliano hayo ulithibitisha kweli Rushwa ya ngono ipo kwenye vyumba vya habari na ni tatizo kubwa ambalo limekua likiathiri utendaji kazi wa taasisi nyingi na ni tatizo mtambuka la jinsia zote mbili, ambapo pia baadhi ya njia za kupambana na tatizo hili zilielezwa ikiwemo umuhimu wa elimu ya jinsia, maadili na sheria.

Miongoni mwa walioongoza majadiliano hayo ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Rose Reuben na Bibie Msumi kutoka Dawati la TAKUKURU.

Leave A Reply