The House of Favourite Newspapers

TANESCO: hali ya upatikanaji umeme kwa sasa Nchini inaelekea kuzuri zaidi

0
Meneja maendeleo na Biashara wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO, Magoti Mtani

Meneja maendeleo na Biashara wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO, Magoti Mtani amesema kuwa hali ya upatikanaji umeme kwa sasa Nchini inaelekea kuzuri zaidi ukilinganisha na kipindi kilichopita cha Shirika hilo

Mtani ameyasema hayo mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye kilele cha Wiki ya Kurasa 365 za Mama Vol. 3 iliyoandaliwa na Clouds Media Group na kusema kuwa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere ujenzi wake umefikia asilimia zaidi ya 93 na pindi likikamilika Megawati 2115 zinategemewa kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa.

Mbali na hiyo ameeleza kuwa Miradi wa Gesi wa Kinyerezi 1 Extension una uwezo wa kuingiza Megawati 180 lakini mwaka huu tayari imeingiza Megawati 160, Mradi wa Maporomoko ya maji Rusumo unaolisha Nchi ya Tanzania, Rwanda na Burundi tayari unalisha Megawati 27 kwenye Gridi yetu ya Taifa.

Leave A Reply