The House of Favourite Newspapers

Tanesco Wapewa Siku 5 Tano Kumaliza Matengenezo

0

WAZIRI wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, ametoa muda wa siku tano kwa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), kuhakikisha linafanya matengenezo ya mtambo wa kufua umeme ili kumaliza tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara katika baadhi ya maeneo nchini.

 

Ametoa maelekezo hayo mkoani Dar es Salaam Machi 2, wakati wa ziara yake katika kituo cha kuzalisha umeme cha SONGAS.

 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dkt Titto Mwinuka, amemhakikishia Kalemani kuwa watasimamia matengenezo ya mtambo huo na hivyo kumaliza tatizo hilo la kukatika kwa umeme katika baadhi ya maeneo nchini.

 

Akizungumzia juu ya kukatika kwa umeme nchini, amesema kuwa kumekuwa na matengenezo ya mitambo mbalimbali kutokana na hitilafu za dharura ambapo alitaja kuwa mitambo iliyo katika matengenezo ni katika vituo vya kuzalisha umeme vya Kidatu, Ubungo I , Ubungo II, Kinyerezi I, Songas  na mitambo ya kuzalisha na kuchakata gesi asilia ya Songosongo.

 

 

Leave A Reply