The House of Favourite Newspapers

TANZANIA YAZIPONGEZA ITALIA, EU KUPIGA VITA YA DAWA ZA KULEVYA

Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, akisoma taarifa yake katika hafla hiyo iliyofanyika  katika ofisi za Ubalozi wa Italia.
Balozi wa Italia Nchini Tanzania, Roberto Mengoni, akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Mmoja wa viongozi wa ubalozi wa Italia akizungumza jambo.

Wakibadilishana jambo.

Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama na Balozi wa Italia Nchini Tanzania, Roberto Mengoni wakikata keki kama ishara ya ufunguzi wa ofisi ya kupiga vita madawa ya kulevya na uhalifu.
Kamishna mkuu wa Mamlaka yaKuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya,Rogers Sianga, akizungumza jambo. 
Wakiendelea kubadilishana jambo.

TANZANIA imezipongeza Italia na Umoja wa Ulaya (EU) kwa ushirikiano wa nchi hizo  katika kupiga vita dawa za kulevya nchini.

 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama,  wakati wa ufunguzi wa ofisi ya kupiga vita madawa ya kulevya na uhalifu ya Umoja wa Ulaya (EU-ACT) jijini Dar es Salaam ambao umefanyika katika ofisi za Ubalozi wa Italia.

 

Katika hafla hiyo, iliyomjumuisha Balozi wa Italia, Roberto Mengoni, waziri Mhagama alisema hatua ya kufungua ofisi hiyo nchini itatoa mchango mkubwa katika kuimarisha uhusiano uliopo wa kupiga vita biashara hiyo  na uhalifu wenye kupangwa kitaifa na kimataifa.

 

“Kama inavyofahamika, sehemu ya kijiografia ya Tanzania inatoa changamoto nyingi katika kupiga vita uovu huo kwani ni moja ya njia kuu katika pwani ya Afrika ambapo madawa haramu ya aina mbalimbali  hupitishwa kuelekea na kutoka Asia Kusini kwenda Ulaya na sehemu nyingine duniani.

 

“Matumizi ya madawa ya kulevya ni tatizo linaloongezeka kila mara na kuwa tishio kwa wananchi kiafya, kijamii, kisiasa, kimazingira na kiuchumi,” alisema Mhagama na kuongeza kwamba, hata hivyo, Tanzania imepiga hatua kubwa katika kukabili janga hili hasa kutokana na kuanzishwa kwa Sheria ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya ya mwaka 2015 iliyozaa mamlaka ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya (DCEA).

 

 

NA DENIS MTIMA/GPL

Comments are closed.