The House of Favourite Newspapers

Tanzia: Chuck Berry Afariki Dunia

Chuck Berry enzi za uhai wake.

MWANAMUZIKI nguli na waanzilishi wa muziki aina ya Rock na Roll, Chuck Berry, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90 nyumbani kwake katika Jimbo la Missouri, huko Marekani.

Chuck Berry enzi za uhai wake.

Muimbaji na mchezaji gitaa huyo alifahamika kote duniani kwa vibao vikali alivyovizindua miaka ya 50s, ukiwemo kibao “Roll Over Beethoven”, ”Sweet Little Sixteen” na “Johnny B. Goode”.

Alianzisha utumiaji wa gitaa wa mchezaji mmoja maarufu kama solos na showmanship kwa wapenzi wa muziki na kuhamasisha bendi kama vile The Beatles na the Rolling Stones.

Comments are closed.