The House of Favourite Newspapers

Tanzia: Mbunge wa Ulanga Mashariki, Celina Kombani afariki dunia

0

kombani1Aliyekuwa Mbunge wa Ulanga Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Celina Ompeshi Kombani enzi za uhai wake.

Aliyekuwa Mbunge wa Ulanga Mashariki mkoani Morogoro kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Celina Ompeshi Kombani amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu huko nchini India.

Akitoa taarifa hiyo ya msiba, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Thomas Kashililah alisema kuwa, marehemu Kombani alikua akisumbuliwa na maradhi ya kisukari na shinikizo la damu hivyo alikwenda nchini India kwa ajili ya matibabu ndipo mauti yakamkuta kule.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa leo kutoka India kuja Tanzania kwa ajili ya mazishi.

Bi. Celina Kombani alizaliwa Juni 19 mwaka 1959 na kufariki leo Septemba 24 mwaka 2015.

Mungua ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi!

Leave A Reply