The House of Favourite Newspapers

Tazama Movies, Tamthilia Mtandaoni Bila Intaneti – Video

0


 

RAHA ILIYOJE! Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika kuendelea kuboresha huduma zake na kuhakikisha linawapa vitu vipya wateja wake hasa katika nyanja ya burudani, limekuja na promosheni ya huduma yao mpya iitwayo TTCL-Burudani (T-Burudani) ambayo imezinduliwa leo Jumanne, Desemba 18, 2019,  katika ofisi za makao makuu ya shirika hilo, Samora Avenue, jijini Dar es Salaam.

 

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba,  amesema TTCL imekuja na ‘application’ mpya ya T-Burudani, itakayomwezesha kila Mtanzania kutazama filamu zenye ubora, tamthlia kali na komedi mbalimbali bure bila kununua wala kuunganishwa na intaneti.

 

Kindamba amesema T-Burudani itawapatia watazamaji wake vionjo na radha ya video mbalimbali za Bongo Movies, Bollywood, Nollywood na nyingine kali kupitia simu zao za mkononi (smart phones, tablets) na kompyuta. Pia, mtazamaji ataweza kupakua na kukodisha filamu azipendazo kwa gharama nafuu kabisa.

“T-Burudani tumeizindua wakati muafaka, hasa ikizingatiwa kwamba katika kipindi hiki cha sikukuu, familia nyingi zinakusanyika pamoja, hivyo ni rahisi kukaa pamoja na kufurahia huku wakitazama movies na filamu kupitia T-Burudani bila intaneti.

 

“Hii ni zawadi ya sikukuu kwa Watanzania, tumetoa ofa kubwa kwa watazamaji watakaopakua app ya T-Burudani kupitia Google Play au App Store ambapo watatazama movies, filamu na comedi bure kabisa kuanzia leo mpaka Desemba 31, 2019, ili wakati huu wa mapumziko watu wa-enjoy,” amesema Kindamba.

 

Vifurushi vya T-Burudani

 

 

Aidha, TTCL imezindua kampeni ya mtaa kwa mtaa kuwafuata Watanzania ili waweze kusajili laini zao za TTCL kwa kutumia mfumo wa alama za vidole kwa mujibu wa sheria ili simu zao zisizimwe kabla ya Desemba 31.

 

“Mimi mwenyewe nitakwenda mtaani kuwahamasisha Watanzania na kuwashawishi kutumia TTCL. Tumeongeza muda wa kufanya kazi Jumatatu mpaka Jumapili, ili wote tuwasajili. Tusingependa kuwaona wanapoteza mawasiliano yao kwa kufungiwa laini zao. Siku ya sikukuu ya Krismasi na ‘Boxing Day’ tutafungua na kuwahudumia wateja wetu. TTCL tumeamua kuhakikisha Watanzania wanapata wanachohitaji,” amemaliza Kindamba.

 

Pakua App ya T-Burudani toka Play Store au App Store au tembelea tovuti ya www.t-burudani.go.tz

Huduma hii ni kwa wateja wa TTCL pekee, Bei zote zinajumuisha gharama za VAT

Kwa maelezo zaidi piga 0222 100 100 au tembelea www.ttcl.co.tz

 

TAZAMA VIDEO YA UZINDUZI HUO

Leave A Reply