The House of Favourite Newspapers

TBL ‘Yamwaga’ Bia Kwenye Vituo Vya Daladala Dar

Wananchi wakiwa katika kituo cha daladala cha Morocco baada ya kuzindua promosheni ya Vuta Pumzi Na Safari Ndogo.

 

Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari Lager imetangaza rasmi promosheni ya Vuta Pumzi Na Safari Ndogo ambapo watumiaji wa bia ya safari watajishindia kinywaji hicho kwenye vituo vya daladala.

 

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Masoko wa Kampuni hiyo, Kabula Nshimo, amesema kuwa promosheni hiyo itahusisha watu walio juu ya miaka 18 na itakuwa siku ya Jumatano pekee.

Akifafanua, Nshimo alisema mtumiaji wa bia hiyo atakwenda kwenye vituo vya daladala/mabasi vyenye huduma hiyo ambayo kwa kuanzia wameanza na kituo cha Morocco na baadaye itasambaa vituo vingine vya daladala ndani ya jiji la Dar es Salaam.

 

Kumbuka mashine hizo zitatoa bia kwa siku ya Jumatano pekee kuanzia saa 10 jioni hadi saa 6 usiku na washindi wote watapelekwa kwenye baa zilizo karibu na kituo husika.

Sikiliza zaidi maelezo ya Nshimo kwenye video hapa chini.

Comments are closed.