The House of Favourite Newspapers

TCAA: Hatujazuia Fastjet Kuingiza ndege, Wanadaiwa Bilioni 6 – Video

Mkurugenzi mkuu wa TCAA, Hamza Johari.

MAMLAKA ya Usimamizi wa Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imesema hawajalizuia Shirika la Ndege la Fastjet Tanzania kuingiza ndege zake Desemba 22, 2018 kama ilivyopangwa na shirika hilo, ikisisitiza kuwa usafiri wa anga haufanywi kwa ujanja.

 

Mkurugenzi mkuu wa TCAA, Hamza Johari.  leo amesema tangu shirika hilo lipewe notisi ya kusudio ya kufutiwa leseni Desemba 17, 2018, liliwasilisha maombi ya uingizaji wa ndege hizo Desemba 24, 2018, na sasa bado mamlaka hiyo inalifanyia kazi.

 

“Madeni ya Fastjet yalikuwa zaidi ya shilingi bilioni sita ambazo wanadaiwa na watu tofauti na tayari wamelipa sehemu ya fedha wanazodaiwa na TCAA japo si zote. Usafiri wa ndege una masharti ya msingi ambayo yasipofuatwa ni hatari,” amesema Johari.

 

“Miongoni mwa mambo ya msingi ni uwezo wa kifedha katika shirika, usafiri wa anga hakuna ujanja kama mhusika hatakidhi masharti kwani  leseni itafutwa.  Tukisema tuhurumiane ni hatari, tutaua watu, usafiri wa anga usiposimamiwa vizuri ni hatari kwa usalama kwani utaua watu.”

Comments are closed.