The House of Favourite Newspapers

Fei Toto, Ngassa Kuivaa Mbeya City

Wachezaji wa timu ya Yanga wakiwa kwenye ndege.

VIUNGO wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Mrisho Ngassa ambao walikosekana katika mechi zilizo­pita za Ligi Kuu Bara, wanatarajiwa kuwepo katika mchezo ujao dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

 

Wachezaji hao walikosekana Yanga kutokana na kutumikia adhabu za kadi walizozipata kwenye michezo iliyopita, lakini baada ya kumaliza adhabu hizo, sasa wapo huru kuitumikia timu hiyo.

Yanga ambayo huu utakuwa mchezo wao wa 18 msimu huu katika ligi, hivi sasa inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 47. Bado haijapoteza hata mechi moja.

 

Mratibu wa Yanga, Hafidhi Saleh, ameliambia Spoti Xtra kuwa, leo Alhamisi kikosi hicho kinaenda Mbeya kikiwa kamili huku Fei Toto na Ngassa nao wakiwa miongoni mwa wasafiri.

 

“Timu inatarajia kuondoka kesho (leo) alfajiri kwenda Mbeya kucheza dhidi ya Mbeya City. Ngassa na Feisal watakuwepo kwenye mchezo huo kwa sababu adhabu zao za kadi zimeisha.

 

“Kwa jumla maandalizi yetu yapo vizuri, Boban (Haruna Moshi) aliumia kwenye mechi ya Kombe la FA, lakini leo (jana) Jumatano amefanya mazoezi na wenzake kama kawaida. Tunataka kuondoka na pointi dhidi ya Mbeya City,” alisema Saleh.

Comments are closed.