The House of Favourite Newspapers

Tchetche atakuwa ghali zaidi Yanga

0

KIPRE.jpg

Straika wa Azam FC, Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast.

Omary Mdose, Dar es Salaam

HUKU straika wa Azam FC, Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast akigoma kurejea nchini kujiunga na wenzake, imebainika kuwa mpango wake wa kutua Yanga upo na atakuwa mchezaji ghali kuliko wote klabuni hapo.

Katika kikosi cha Yanga hivi sasa, Mzambia, Obrey Chirwa ndiye ghali zaidi baada ya usajili wake kugharimu zaidi ya Sh milioni 200.

Hivi karibuni uongozi wa Azam ulitangaza kama kuna timu inamuhitaji straika wao huyo, iende mezani kwao kuzungumza na wakikubaliana basi watamuachia kwa moyo mmoja.

Azam ilisema thamani ya Muivory Coast huyo ni dola 150,000 ambazo ni zaidi ya Sh milioni 300.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa kwa sasa hivi mipango inafanywa kuhakikisha Tchetche anakuwa mchezaji wao, lakini watamaliza kila kitu katika usajili wa dirisha dogo hapo baadaye.

Championi lilipozipata taarifa hizo, likamtafuta Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit, ambaye kwanza alishtuka kusikia taarifa hizo na kudai kuwa ndiyo kwanza anazisikia lakini akabainisha kwa sasa hawana mpango naye labda hapo baadaye.

“Hizo taarifa bado sijazipata, lakini ukiangalia hivi sasa kikosi chetu kina wachezaji saba wa kigeni ambao ndiyo wanaotakiwa kwa mujibu wa TFF (Shirikisho la Soka Tanzania), hivyo hakuna nafasi yake labda hapo baadaye,” alisema Deusdedit.

Wachezaji wa kigeni wa Yanga ni Chirwa raia wa Zambia, Amissi Tambwe (Burundi), Vincent Bossou (Togo), Thabani Kamusoko na Donald Ngoma (wote Zimbabwe), Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite (wote Rwanda).

 

Leave A Reply