Tecno Kutoa Mil. 1 kwa Mshindi Promosheni ya Tecno ‘Camon 16 Billboard Star’

Picha ya msanii LULU ikionesha namna mwonekano wa picha ya mshindi wa Camon16 Billboard Star itakavyokaa kwenye bango.

Kampuni ya simu za mkononi ya TECNO imetangaza kuanza rasmi promosheni ya Camon16 Billboard Star ambayo itawawezesha wafuasi wake wa kurasa za mtandani pamoja na wateja kwa ujumla kujinyakulia zawadi ya  kitita cha shilingi milioni moja, kupata nafasi ya kuwekwa kwenye bango kwa muda wa wiki kadhaa pamoja na kupata nafasi ya kwenda ziara ya Camon 16.

 

Akizungumza wakati wa kuitambulisha kampeni hiyo jijini Dar es Salaam, meneja masoko mtandaoni Bi. Salma Shafi amesema wameandaa kampeni hiyo maalum kwaajili ya wateja na wafuasi wao wa kwenye kurasa zao mtandaoni.

 

“Hii ni kampeni ambayo inamtaka mshiriki kupiga picha yoyote kwa ubunifu yaani ‘creative photo’                            Picha inaweza kuwa ya mtu au kitu yenye ubunifu kwa kutumia TECNO CAMON 16 au simu yoyote ya toleo la TECNO CAMON na ahakikishe ameweka water mark ili kutambulisha picha imepigwa kwa simu ya toleo la TECNO CAMON. Akishapiga picha anatakiwa aposti kwenye akaunti yake ya Instagram kwa hashtag #Camon16BillboardStar” amesema Bi. Salma

Picha ya mtangazaji Omary Tambwe ikionesha namna mwonekano wa picha ya mshindi wa Camon16 Billboard Star itakavyokaa kwenye bango

 

Bi. Salma ameongeza kuwa Kupitia kampeni hiyo ya ‘Camon 16 billboard star’ ambayo itadumu kwa muda wa wiki moja na mwishowe watachaguliwa washindi watano na kuwa reposted kwenye ukurasa wa  Instagram ‘tecnomobiletanzania’ kisha kufanyiwa mchujo kwaajili ya kupata mshindi mmoja.

Picha ya Miss University Jihan Dimack Ikionesha namna picha ya mshindi wa itakavyokaa kwenye bango

Kampeni hiyo ya Camon16 Billboard Star, itafuatana na ziara ya Camon16 ambapo washindi watapata nafasi ya kutembelea maeneo mbalimbali ya hifadhi za Taifa ikiwemo Hifadhi ya Ngorongoro.

 

Je, ungependa kufahamu zaidi kuhusu promosheni hii?  Tafadhali tembelea ukurasa wa TECNO Instagram kwa kubofya link hii;   https://www.instagram.com/tecnomobiletanzania/

Toa comment