The House of Favourite Newspapers

TECNO waja na matoleo mapya makubwa matatu

Meneja wa Boomplay, Natasha akizungumza wakati wa uzinduzi huo

Kampuni ya simu za mkononi ya Tecno imewanufaisha wateja wake kwa kuja na matoleo mapya makubwa matatu ya simu hizo ambayo ni TECNO Camon 12, Camon 12 air na Camon 12 pro huku wakiwa na kauli mbiu mpya ya TECNO EXPERT MORE. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jana, Ofisa Uhusiano wa TECNO Mobile Tanzania, Eric Mkomoye alisema kwamba;

“Mageuzi ya kiteknolojia kutoka analojia kwenda digitali yanawezekana kama sifa zote zinazohitajika zinapatikatana kiganajani mwako kama vile kamera nzuri, betri nzuri na yenye nguvu, uwezo mkubwa wa kuhifadhi data pamoja na muonekano wa kipekee.”

Viongozi wa Tecno wakiwa wameshika simu hizo wakati wa uzinduzi

Mkomoye aliorodhesha sifa za TECNO Camon 12 kama ifuatavyo; “16MP +2MP+8MP Rear camera with quad flash, 16MP Al Clear Selfie, GB64+GB4, 400mAh battery, 6.52 screen na 4G ambazo ni Android 9 Pie.” Katika uzinduzi huo, mmoja wa mawakala wa TECNO na mdau, Abuyi alisema furaha yake ni kuiona TECNO ikipiga hatua zaidi na kufanikiwa katika soko.

wadau wakiwa ukumbini kwenye uzinduzi huo

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wadau kutoka sekta mbalimbali mfano, masoko, mauzo na teknolojia. Alikuwepo pia Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, George Mathen, Ofisa Masoko wake, Amit Chandiramani, Mkurugenzi Mtawala wa TIGO, Simon pamoja na Ofisa Masoko  wa Vodacom Tariq. Tofauti na hilo, shughuli nyingine ya burudani ilikuwepo pamoja na droo ya kubahatisha ambapo wageni waalikwa walipata nafasi ya kujishindia simu aina ya TECNO Camon 12 papo kwa hapo.

 Matukio katika Picha:

Wadau wakielekezwa namna simu hiyo inavyofanya kazi

Imeandaliwa na Neema Adrian/GPL

Comments are closed.