The House of Favourite Newspapers

Vodacom yanyakua tuzo DSE

Mkuu wa Uhusiano wa Uwekezaji na Miradi Maalumu wa Vodacom Plc, Robin Kimambo akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo.

Kampuni inayoongoza kwa teknolojia ya mawasiliano nchini Tanzania, Vodacom imeshinda tuzo ya soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Hafla ya kukabidhi tuzo hizo ilifanyika juzi jijini Dar es Salaam, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni  ‘Mazingira, Jamii na Utawala Endelevu’ ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.  Ashatu K. Kijaji.

Lengo kuu la tuzo hizo ni kukuza ubora wa biashara katika nyanja ya Utunzaji wa Mazingira, Utawala Bora wa Kampuni, Kuongeza Uwajibikaji katika shughuli za Kijamii na kuhakikisha kuwa DSE inaendelea kutimiza wajibu wake kwa wanachama.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kulia) akikabidhi tuzo ya Kampuni Bora DSE kwa mwaka 2019 , kwa Mkuu wa Uhusiano wa Uwekezaji na Miradi Maalumu wa Vodacom Plc, Robin Kimambo

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkuu wa Uhusiano wa Uwekezaji na Miradi Maalumu wa Vodacom Plc, Robin Kimambo, alisema tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa kampuni hiyo ambayo kwa sasa inaongoza kwa uvumbuzi kwenye teknolojia ya mawasiliano nchini.

“Jambo la msingi ni kuwaahidi watanzania kuwa, tutaendelea kuwa wabunifu na wavumbuzi ili kuendelea kutoa huduma ambapo kwa sasa tuna takriban wateja zaidi ya milioni 14 nchi nzima,” alisema.

Tuzo waliyoipata Vodacom

 

Washiriki wa tuzo hizo ni kampuni zilizoorodheshwa DSE ambazo ni pamoja na Madalali au Wafanyabiashara, Washauri waliopendekezwa pamoja na vyombo vya habari vya kidigitali na magazeti Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc iliorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam Agosti 15, 2017.

 

Imeandaliwa na Neema Adrian/GPL

Comments are closed.