The House of Favourite Newspapers

TECNO WAZINDUA TECNO Spark 4

Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Tigo, Mkumbo Mnyonga (katikati) akiongea kwenye uzinduzi wa simu mpya aina ya TECNO Spark 4.

KAMPUNI ya simu ya TECNO kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya  Tigo jana wamezindua simu mpya aina ya TECNO Spark 4 yenye sifa inayouzwa kwa bei nafuu sana.

Akizungumza na wanahabari kwenye uzinduzi wa simu hiyo uliofanyika katika duka la TECNO Spark Hub lililopo Kariakoo, Dar es Salaam, Meneja Masoko wa kampuni hiyo, William Motta,  alisema teknolojia iliyopo kwenye simu hiyo inazipa uwezo kamera za nyuma GB 32 za memory na kioo cha nchi 6 full –view. Pia simu hizo betri zake zinadumu na chaji kwa muda mrefu.

Wakati huohuo Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa  Tigo, Mkumbo Mnyonga,  alisema wateja watakaponunua simu hiyo watazawadiwa ofa ya GB 18.

 

Matukio katika Picha:

Afisa Uhusiano wa Tecno, Eric Mkomoye (kushoto) akitoa ufafanuzi kwenye uzinduzi huo.
Wadau wakifuatilia uzinduzi wa simu hiyo kwenye skrini.
Wahudumu wa TECNO wakiwaelekeza wateja matumizi ya simu hiyo.
Boksi la simu hiyo linavyoonekana.

 

HABARI/PICHA: NEEMA ADRIAN / GPL  

 

 

 

Comments are closed.