The House of Favourite Newspapers

TECNO YATIMIZA NDOTO ZA WATOTO YATIMA

                                             

Katika kuhakikisha jamii ya Kitanzania inafanikiwa na kufaidika kwa uwepo wake Kampuni ya simu nchini Tanzania TECNO Mobile yahakikisha zaidi ya watoto 100 ambao ni yatima wanapata vifaa vya shule.

 

 

TECNO imefanikiwa kuchangia fedha pamoja na mahitaji mengine ya msingi kwa kituo cha Chanika Children Shelter kinacholea watoto yatima kilichopo chanika, jijini Dar es Salaam, katika kituo hicho takribani watoto wenye umri tofauti kuanzia miaka 4 mpaka 18 wanaolelewa kwa usaidizi mkubwa wa mmiliki wa kituo hicho kiongozi wa madhehebu ya budha nchini Dkt. Pannasekara.

Akizungumza wakati wa makabidhiano  meneja  uhusiano wa Kampuni ya simu ya TECNO, Erick Mkomoye alisema kwamba, “ndoto za Watoto hao ndio zilizopelekea kampuni ya simu ya TECNO kuanzisha kampeni inayofahamika ‘KUWA SHUJAA WANGU’  kwa kuchangia hundi ya kiasi cha millioni 5 ili kutimiza mahitaji yao ya shule,  tuliwashawishi watanzania na wateja wetu kuwasaidia watoto hawa kadri wawezavyo lakini pia sisi kama kampuni pia tutawasaidia watoto hawa kuhakikisha ndoto zao zinatimia tumeanza na million 5 na tutaendelea. ”

Bwana Eric aliongeza, “KUWA SHUJAA WANGU ni kampeni ambayo imepelekea kuwasaidia watoto wa Chanika Children Shelter ili kutimiza ndoto zao za kwenda shule na kuanza masomo yao katika ngazi tofauti tofauti  sekondari na msingi na hata chekechea  ili baadaye waje timiza ndoto kubwa zaidi za  kuwa daktari, mwalimu, rubani katika kulifanikisha hili TECNO tumeamua kuipa muendelezo kampeni hii kwa mwaka wote huu wa 2019”.

Comments are closed.