The House of Favourite Newspapers

TEMBO WA HARMO AZUA BALAA

0

VITA ya panzi majani ndiyo yanayoumia! Unaweza kutumia msemo huu kutokana na staa wa muziki wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ kuonekana akiwa amechora tattoo ya tembo mgongoni na kuzua balaa kwa kile wengi walichodai kuwa amemjibu Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye anayo ya simba.

Harmo alizua balaa la aina yake baada ya picha yake hiyo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram ambapo wengi waliyoiona walidai kuwa amemjibu Diamond kwamba yeye ni tembo ambaye ni mkubwa kuliko simba.

Wengine walienda mbali zaidi na kumuonya Harmo kuwa awe makini na aweke akili yake kwenye kazi yake ya muziki zaidi kuliko kufanya mashindano au malumbano na Diamond kwani hawezi kumshika, amemwacha mbali sana kimuziki hata kimafanikio binafsi.

“Yaani huyu Harmo akiendelea kumjibu au kumuiga kila kitu Diamond atapotea kabisa kwenye ulimwengu wa muziki, anatakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuachana na mambo haya ambayo hayana msingi.

“Sasa ona hapa amejichora tattoo ya tembo kumfikishia ujumbe Diamond kuwa yeye ni mkubwa kuliko yeye ambaye anajiita simba na amejichora tattoo ya mnyama huyo,” alisema mmoja wa wadau mtandaoni humo.

HARMO ANASEMAJE?

Kutokana na balaa hilo lililozuka mtandaoni humo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Harmo kwa njia ya simu kupitia kwa meneja wake, Beauty Mmary ‘Mjerumani’ ili kumuuliza kwamba ni kweli Harmo amemjibu Mondi kwa tattoo hiyo ya tembo, lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

Hata alipotafutwa kwa njia ya Mtandao wa WhatsApp na kuelezwa juu ya hilo, alisoma maelezo hayo na kukaa kimya bila kujibu chochote

 

STORI: GLADNESS MALLYA, RISASI

Leave A Reply