The House of Favourite Newspapers

TETEMA ya Rayvanny na Diamond Yapigwa Marufuku

WIMBO Tetema wa msanii Raymond Mwakyusa maarufu Rayvanny aliomshirikisha Diamond Platnumz umepigwa marufuku kupigwa katika maeneo ya wazi nchini Kenya.

 

Mbali na Tetema, wimbo mwingine uliopigwa marufuku kupigwa maeneo hayo ni Wamlabez wa msanii Sailors wa nchini Kenya.

 

Kiongozi wa Bodi ya Filamu nchini Kenya (KFCB), Ezekiel Mutua,  amesema sababu ya kuzizuia nyimbo hizo ni kuwa na maudhui yanayokwenda kinyume na maadili.

 

“Nyimbo za Tetema na Wamlambez zinazuiwa kuchezwa nje ya vilabu na baa. Inatia aibu kuwaona hata viongozi wa kitaifa wakidensi na kuimba nyimbo za aibu mbele ya hadhara.

“Maneno katika nyimbo hizo ni uchafu na hayafai kusikilizwa hadharani hususan mahali ambapo kuna watoto wanaoweza kuwa wanasikiliza maneno au kuona mtu akicheza. Nyimbo zote mbili ni ponografia halisi ,” ameandika Mutua.

 

“Japo hatuzipigi marufuku kwa sababu zinaimbwa kwa mtindo wa mafumbo, ni muhimu kwa umma kufahamu kuwa nyimbo hizi ni chafu, na hazifai kuchezwa mahali penye mchanganyiko wa watu wa rika tofauti. Acha zipigwe kwenye vilabu, kwa ajili ya watu wazima pekee!” aliandika.

 

Hata hivyo,  haijafahamika ni vipi agizo la  Mutua litatekelezwa na bodi ya udhibiti wa maudhui ya kiusanii.

Comments are closed.