The House of Favourite Newspapers

TFF ya Botswana Wairahisishia Kazi Yanga

WAKIJIANDAA na mchezo wa marudiano dhidi ya Township Rollers, Yanga wamepewa uwanja wa kufanyia mazoezi na Shirikisho la Soka la Botswana.

 

Hiyo ni siku moja imepita tangu timu hiyo itue kwenye mji wa Gaborone huko nchini Botswana ambako watacheza mchezo wao wa marudiano Jumamosi hii saa 10:30 jioni. Timu hizo kwenye mchezo wa awali uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema kuwa wameshukuru mapokezi waliyoyapata mara baada ya kutua nchini.

Aliongeza kuwa wanautumia uwanja huo wa nyasi bandia baada ya kupata taraifa za mchezo huo kuchezewa katika uwanja wa nyasi bandia.

 

“Kama nilivyokwambia awali kuwa sisi viongozi tuliwahi kufika mapema na malengo kuweka mazingira mazuri ya timu kufikia, pia kuandaa uwanja mzuri tutakaotumia kwa ajili ya mazoezi.

 

“Hivyo, mara baada ya kufika hapa Botswana mimi nilifanya jitihada za kutosha kuhakikisha timu inafikia hoteli nzuri na uwanja wa mazoezi.

 

“Katika hilo tulifanikiwa tumepata hoteli nzuri na uwanja wa nyasi bandia ambao tutautumia kwenye mchezo huo wa marudiano na tunatumia uwanja wa aina hiyo ni baada ya kupokea mapendekezo ya kocha wetu Zahera,”alisema Mwakalebela.

EXCLUSIVE NA PACHO MWAMBA AFUNGUKA, KANUMBA, MAMA KANUMBA,

Comments are closed.