The House of Favourite Newspapers

TFF Yasaini Mkataba wa Miaka 3 na Serengeti

0

SHIRIKISHO  la Soka Tanzania, (TFF) chini ya Rais Wallace Karia, leo Oktoba 6, 2020,  limeingia makubaliano na Bia ya Serengeti Premium Lager na kusaini mkataba wa kuidhamini timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwa kipindi kingine cha miaka mitatu.

Makubaliano hayo yamefanyika mbele ya wanahabari katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo pia jezi mpya za timu hiyo zimezinduliwa.

Mkataba huo ni wa miaka miatu wa kiasi cha shilingi bilioni 3 za Tanzania.

Kwa sasa timu hiyo ipo kambini ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya shirikisho la soka duniani (FIFA) dhidi ya Burundi utakaochezwa Oktoba 11, Uwanja wa Mkapa.

WAZIRI MWAKYEMBE Azindua UKUMBI wa MATAMASHA – “Hata JAY Z Anaweza KUJA Hapa AKAPIGA SHOO”

Leave A Reply