The House of Favourite Newspapers

TGNP Ilivyotoa Elimu ya Kushiriki Kutunga Bajeti na Kutatua Changamoto Kwenye Jamii

0
Mwezeshaji kwenye warsha hiyo, Deogratius Temba akitoa somo.

 

 

Mtandao wa Jinsia nchini (TGNP) umewanoa wanahabari na viongozi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa kwenye warsha ya siku mbili Juni 28 mpaka 29 ambayo ilihusu suala la ushiriki wa mchakato wa kutunga bajeti kuanzia ngazi ya kitongoji kijiji mpaka halmashauri na kwa mijini kuanzia ngazi ya mtaa. Pamoja na kufundishwa suala la kushiriki upangaji wa bajeti kuanzia ngazi za chini kabisa waliibuliwa wanahabari kwenye jamii kwa ajili ya kuongeza wigo wa upatikanaji wa habari na uibuaji kiurahisi na haraka wa changamoto zilizopo kwenye jamii.

Deogratius Temba akiendelea kutoa somo.

 

 

Warsha hiyo ilihusisha washiriki kutoka kata ya Saranga, Kivule, Mabwepande na Majohe zilizopo Dar na Kata ya Kiloleni iliyopo mkoani Shinyanga ambao walieleza changamoto ambazo waliwahi kuzishughulikia kwenye maeneo yao kama viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa.

Kiongozi wa kituo cha taarifa na maarifa Bi. Wangu Limbu kutoka Kata ya Kiloleli, akieleza changamoto walizopambana nazo eneo hilo.

 

 

KILOLELI – SHINYANGA

Akizungumza kwenye warsha hiyo mwenyekiti wa kituo cha taarifa na maarifa Kata ya Kiloleli mkoani Shinyanga, Bi. Kwangu Limbu amesema awali alipopatiwa mafunzo na TGNP alirudi kwenye kata hiyo na viongozi wenzake na kushungulikia changamoto za maji, elimu, afya, ukatili wa kijinsia na mengineyo.

 

 

Kwangu amesema awali suala la maji lilikuwa tatizo kubwa kwao ambapo mpaka sasa bado wanatumia maji ya bwawa ambalo mchana wanatumia ng’ombe na mifugo mingine usiku ndiyo wananchi wanapata nafasi ya kuchota maji. Kwangu amesema licha maji hayo kutokuwa salama lakini bwawa hilo liko mbali sana na wanapoishi ambapo wanawake wanapofunga safari ya kwenda kuchota maji saa mbili usiku wanafika nyumbani saa mbili asubuhi, amesema Bi. Kwangu.

Washiriki wakisikiliza kiumakini.

 

 

Ameendelea kusema changamoto hiyo imewasababishia majanga mbalimbali ikiwemo wanawake kubakwa wakiwa njiani nyakati za usiku, kuvunjika kwa ndoa zao, mimba za utotoni na mengineyo. Amesema kutokana sauti walizopaza baada ya kupata mafunzo ya TGNP wameshirikiana na viongozi wa serikali kuibua chamoto hiyo ambapo sasa bwawa hilo limetengewa fedha kwa ajili ya kuboresha na kusambaza maji safi na salama kwa wakazi wa Kiloleli.

Kiongozi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Mabwepande, Fatuma Nuru naye akieleza jinsi walivyoibua changamoto eneo hilo na mafanikio waliyofikia.

 

 

Kuhusu changamoto ya elimu Kiloleli,  Kwangu amesema hapo awali walimu walikuwa na changamoto nyingi ikiwemo uhaba wa vifaa vya kufundishia, madarasa na walimu kukosa nyumba za kuishi. Kwangu amesema kuna shule moja hapo Kiloleni kulikuwa na mwalimu ambaye alikuwa akilala ofisini jambo ambalo lilikuwa likimuathiri kisaikolojia na kumfanya ashindwe kutimiza majukumu yake kiufasaha.

Mwandishi wa gazeti la Habari Leo kituo cha Shinyanga Kareny Masasy akisiliza kiumakini yanayoendelea.

 

 

Ameendelea kusema kuwa yeye na viongozi wenzake wa kituo cha taarifa na maarifa eneo hilo walimpigania mwalimu huyo na kufanikisha kupatatikana kwa wadau na kumjengea nyumba nzuri ya kuishi na familia yake.

Kiongozi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Saranga, Anjela Mfinanga naye akielezea changamoto walizoibua na kuzipatia ufumbuzi.

 

 

SARANGA- DAR

Kiongozi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Saranga, Bi. Anjela Mfinanga amesema awali baada ya kupatiwa mafunzo ya kuibua changamoto za jamii alishirikiana na wanahabari na viongozi wa kata na serikali za mitaa na kufanikiwa kumaliza mgogoro wa soko uliokuwa ukifukuta kwenye eneo hilo.

Mwezeshaji Speratus Kyaruzi kutoka TGNP akiwapa somo washiriki.

 

 

Anjela amesema sasa hivi wanafuatilia changamoto ya rushwa ya ngono katika ugawaji wa vizimba vya kufanyia biashara ambapo taarifa za chinichini zinadai kwenye soko hilo mwanamke akitaka kupata kizimba cha kufanyia biashara ni lazima atoe rushwa ya ngono, amesema Anjela.

Mwandishi wa Malunde 1Blog, Kadama Malunde akiwa kwenye warsha hiyo.

 

 

MABWEPANDE, MAJOHE NA KIVULE- DAR

Viongozi wa Taarifa na Maarifa wa Kata za Mabwepande, Majohe na Kivule kwa kushirikiana na viongozi wa mitaa na kata wao walieleza jinsi walivyoshughulia tatizo za maji kwenye maeneo hayo ambapo sasa maeneo yote hayo yameshafikiwa na mradi wa maji na mabomba tayari yameshaanza kusambazwa na maji yameshaanza kutiririka baadhi ya maeneo hayo. Upande wa elimu elimu na kwenyewe wameibua changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa matundu ya vyoo ambapo sasa yote hayo yameshaanza kupatiwa ufumbuzi baada ya kutengewa bajeti ya serikali. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply