The House of Favourite Newspapers

TGNP Yawapiga Msasa Wanahabari, Makundi Mengine

0

                                                                                                                                                                                 

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akifungua warsha hiyo kwa wanahabari.

 

Mtandao wa Jinsia TGNP leo umeanza warsha wa siku mbili kwa ajili ya kuwapa uwezo Wanahabari na Viongozi wa Vikundi ya Taarifa na Maarifa kutoka mikoa mbalimbali kuhusiana na masuala ya bajeti yenye mrengo wa kijinsia.

 

Akifungua warsha hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi amewaambia washiriki hao kuwa suala la kijinsia ni la kimaendeleo hivyo kunapokuwa na utengwaji rasilimali ambazo zinaangalia kwa mtazamo wa kijinsia maana yake makundi yote yatanufaika na rasirimali za taifa.

Afisa Habari wa TGNP, Monica John akitoa muongozo kwa washiriki hao (hawapo pichani).

 

 

Mkurugenzi Lilian amesema mfano katika mageuzi ya sekta ya kilimo ambayo wanawake wanahusika kwa asilimia 80 ikiboreshwa na kumuangalia mwanamke kwa uzito mkubwa tutajipatia mafanikio ya haraka na makubwa.

 

Mkurugenzi huyo ameendelea kusema;

“Katika sekta za uchumi upande wa madini, utalii, viwanda, teknolojia ya habari na mawasiliano zimekuwa zikimuweka pembeni sana mwanamke, hivyo tunatarajia awamu ya 6 usawa utaangaliwa ili makundi mbalimbali kama vile vijana, wanawake, walemavu na makundi mengine yaweze kufaidika.

Mkurugenzi Lilian Liundi akitoa somo kwa washiriki.

 

“Kwenye sekta za huduma kama vile elimu, maji, afya, nishati nazo zimepewa uzito mkubwa” amesema Mkurugenzi huyo.

 

“Upande wa sera elimu, Mheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan amesema itapitiwa vizuri ambapo mtoto wa kike ambaye alikuwa akikabiliwa na changamoto nyingi nayo itapatiwa ufumbuzi,” amesema Mkurugenzi Lilian.

Mwandishi wa Habari Leo kutoka mkoani Shinyanga, Kareny Masasy akitoa mawazo yake kwenye warsha hiyo.

 

Upande wa afya, Mheshimiwa Mama Samia amesema amekerwa na vifo vya wanawake wakati wa kujifungua na kuahidi kuimaliza changamoto hiyo.

 

Mama ndiye anayewaleta wachapakazi duniani ambao ni rasirimali watu hivyo nafasi yake ni muhimu sana katika suala la maendeleo. Alisema Mkurugenzi Lilian.

 

Baada ya kusema hayo mwezeshaji katika warsha hiyo, Deogratius Temba aliwawezesha washiriki kutambua changamoto za usawa wa kijinsia na kutoa mifano mbalimbali akijadiliana na washiriki hao.

Mtangazaji wa moja ya redio zilizopo mkoani Shinyanga aliyejitambulisha kwa jina la Moshi akiuliza swali kwenye warsha hiyo.

 

Katika warsha hiyo, washiriki walijadiliana mambo mbalimbali kuhusiana na bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

HABARI/PICHA:RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply