The House of Favourite Newspapers

Thaban Kamusoko, Papy Tshishimbi Wapewa Viatu Maalum

Papy Kabamba Tshishimbi.

DAKTARI wa Yanga, Edward Bavu ameshauri kiungo nyota wa klabu hiyo, Papy Kabamba Tshishimbi atumie viatu visivyokuwa na meno chini ‘training shoes’. Alichofanyiwa staa huyo ni sawa na Thaban Kamusoko ‘Kampa kampa tena’ na Obrey Chirwa.

 

Uamuzi huo umetoka baada ya Mkongomani huyo kuruhusiwa kuanza kuuchezea mpira akitokea kwenye majeraha ya kifundo cha mguu yaliyomuweka nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili nje.

Tshishimbi aliyetua Yanga akitokea Mbabane Swallows ya Swaziland, akiwa anauguza majeraha alizikosa mechi za ligi dhidi ya Mtibwa Sugar na Mbeya City.

Thaban Kamusoko.

Bavu ameiambia Spoti Xtra kuwa mchezaji huyo tegemeo,atatumia viatu hivyo kwenye mazoezi ya timu pekee kwenye Uwanja wa Uhuru uliopo jijini Dar es Salaam.

 

Alisema mazingira ya uwanja huo wa Uhuru ndiyo yamesababisha kiungo huyo atumie viatu hivyo kwani sehemu yake ya kuchezea ni ngumu kama akiendelea kuvaa njumu, basi atajitonesha kila siku.

 

Aliongeza kuwa, wapo baadhi ya wachezaji kama Obrey Chirwa na Thabani Kamusoko wenyewe muda mrefu wanatumia viatu hivyo maalumu visivyokuwa na meno.

 

“Uwanja huu wa Uhuru tunaotumia kwa ajili ya mazoezi kiukweli siyo mzuri kwa afya za wachezaji wetu kwani unasababisha majeraha yasiyokuwa na lazima.

 

“Kwani sehemu ya kuchezea ni ngumu sana kutokana na nyasi zake bandia kukakamaa hali inayosababisha wachezaji wangu kupata majeraha kila siku, lakini hatuna jinsi tunalazimika kuutumia kwani hatuna uwanja mwingine.

 

“Hivyo, basi tayari nimewataka wenye majeraha kutotumia njumu na badala yake watumie vile visivyokuwa na meno chini kwa hofu ya kupata majeraha mapya au kujitonesha kama ilivyokuwa kwa Tshishimbi ambaye yeye nimemwambia atumie viatu hivyo,”alisema Bavu.

 

Yanga inajiandaa na mechi za ligi pamoja na Kombe la Mapinduzi linaloanza hivi karibuni mjini Unguja.

STORI: WILBERT MOLANDI | GLOBAL PUBLISHERS

Comments are closed.