The House of Favourite Newspapers

Thea, Mike…. Mahaba Kama Yote

0

MAHABA kama yote! Mastaa wawili ambao waliokuwa wanandoa kabla hawajamwagana, Salome UrassaThea’ na Michael Sangu ‘Mike’ hivi sasa ni mahaba niue, Risasi Jumamosi linakupa habari kamili.

 

Wawili hao walinaswa hivi karibuni wakioneshana mahaba upya ndani ya Hoteli ya Sea Cliff, Masaki jijini Dar ambako kulikuwa na chakula cha jioni kwa wanahabari wa vyombo mbalimbali ‘Media Dinner’ kilichoandaliwa na Swahili Flix.

 

Wakati shughuli hiyo iliyohudhuriwa na wasanii mbalimbali wa filamu ikiendelea, Mike na Thea wao walikaa meza moja huku kila wakati wakioneshana mahaba mara wanong’onezane, mara waoneshane vitu kwenye simu yaani ilikuwa fulu furaha kwao.

 

Kutokana na kuoneshana mahaba huko, watu mbalimbali walionekana wakiwapiga chabo kwani wapo ambao hawakuwa wakiamini macho yao kwa sababu wawili hao kila mmoja alishasema kwamba hawawezi kuwa pamoja tena.

 

“Jamani kweli mapenzi ni kitu cha ajabu, hawa walishasema hawawezi kuwa pamoja tena lakini leo naona wanaoneshana mahaba kama yote, hawa watakuwa wamerudiana, siyo bure,” alisema mmoja wa wasanii ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini aliyekuwa kwenye shughuli hiyo.

 

Risasi Jumamosi liliwafuata wawili hao na kuzungumza nao ambapo Mike ndiye aliyekuwa akijibu huku akicheka.

“Ahahahaha jamani hapa tunapanga jinsi ya kufanya projekti na hakuna kitu kingine, hatuzungumzii suala la ndoa,” alisema Mike huku akicheka.

 

Thea na Mike walikuwa wanandoa ambapo ndoa yao ilivunjika mwaka 2015 huku kila mmoja akieleza kuwa hawezi kuweka wazi chanzo ni nini.

 

Mara kadhaa wawili hawa wamekuwa wakionekana kwenye mitoko tofautitofauti lakini hawakuoneshana mahaba kama ambayo wameoneshana kwenye media dinner na kuzua gumzo kwamba huwenda wawili hawa wanaweza kurudiana jumla na wakaishi kama mke na mume.

Leave A Reply