The House of Favourite Newspapers

Thierry Achemka Monaco

KOCHA wa Monaco, Thierry Henry anakabiliwa na presha kubwa kutokana na timu yake kuboronga kwenye Ligue 1. Monaco ilicharazwa mabao 4-0 na Paris Saint- Germain, wikiendi iliyopita kwenye mechi ya Ligue 1.

 

Henry anakabiliwa na wakati mgumu kutokana na timu hiyo kuboronga kwenye Ligue 1 na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

Straika huyo, ambaye alianzia soka yake katika timu ya watoto ya Monaco, amekuwa na bahati mbaya ya timu yake kuwa na majeruhi wengi. Monaco ilijikuta ikipokea kipigo cha pili mfululuzo baada ya kufungwa na Club Brugge ya Ubelgiji kwenye makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

Katika mechi dhidi ya PSG, mabao matatu yalipachikwa na Edinson Cavani wakati Neymar alifunga kwa penalti. PSG Inaongoza kwa pointi 13 kwenye Ligue 1, wakati Monaco ipo kwenye nafasi za mkiani kwenye ligi hiyo.

MONACO, Ufaransa

Comments are closed.