The House of Favourite Newspapers

Thomas Ulimwengu Aondoka TP Mazembe, Sasa Kuzisaka Klabu za Ulaya

mazembeKlabu ya TP Mazembe ya Jahmhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo alikuwa akiichezea Mtanzania, Mbwana Samatta anayekipiga kunako Ubelgiji, jana Oktoba 23, 2016 ilitangaza rasmi kupitia tovuti ya klabu hiyo kuwa mchezaji wake Mtanzania, Thomas Ulimwengu amemaliza mkataba na TP Mazembe, lakini Ulimwengu hajataka kuongeza mkataba mwingine.

ulimwenguTP Mazembe kupitia tovuti yao wameeleza kuwa Ulimwengu amemaliza mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia klabu hiyo, lakini wameweka wazi kuwa walimuhitaji lakini Ulimwengu amekataa kufanya mazungumzo ya kuongeza mkataba na anataka kuondoka.

Inasemekana Ulimwengu amekataa mazungumzo na TP Mazembe ili awe huru kuelekea Ulaya ili kutafuta timu ya kuichezea Barani huko.

Comments are closed.