The House of Favourite Newspapers

Tiba ya Kuvimba kwa Fizi

Viazi Mbatata

WATU wengi hupatwa na ugonjwa wa kuvimba fizi na wakati mwingine fizi hizo hupatwa na usaa kutokana na uvimbe. Leo nimewaletea tiba ambayo inaweza kukusaidia ukapona na kusahau maumivu yote.

Viazi mbatata ni tiba nzuri ya tatizo la kuvimba kwa fizi unachotakiwa kufanya ni kukata kipande cha kiazi mbatata na kukiweka eneo lililoathirika, kiazi hiki huondoa maambukizi unachotakiwa ni kutumia kiazi hiki usiku kucha.

Maji

Kunywa maji mengi, hii ni dawa tosha itakusaidia kwa asilimia kubwa kuondoa maumivu, jitahidi kunywa maji glasi 3 ili kuondoa maumivu.

Baking soda na chumvi

Unaweza kuandaa

mchanganyiko wa baking soda na chumvi kisha chukua pamba chovya baada ya hapo weka kwenye fizi inasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa maumivu, unachotakiwa ni kurudia tiba hiyo mara kwa mara kwa wakati huo na kila baada ya masaa mawili.

Mafuta ya karafuu na Hydrogen Peroxide

Chukua mafuta ya karafuu changa-nya na hydrogen peroxide (hii ni dawa ya kusuku-tua ya vidonda). Ukim-aliza chukua pamba

chovya kwenye mchanganyiko huo kisha weka kwenye ufizi wako uliovimba.

Vitamin C

Ukiona fizi yako imeanza kuvimba kabla haija-toa usaha hakik-isha unakula Vitamin C hasa machungwa.

Lakini pia unaweza kutumia kitunguu swaumu kitakusaidia.

Na Hamida Hassan

Comments are closed.