TIFFAH AIWEKA PABAYA FAMILIA MONDI

DAR ES SALAAM: MTOTO wa nyoka ni nyoka! Ndivyo unavyoweza kusema. Kama ilivyokuwa kwa baba yake, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa kinara wa kuzalisha matukio ya kihabari za mastaa, vivyo hivyo imekuwa kwa mwanaye Tiffah ambaye pia amezalisha tukio la kuiweka pabaya familia ya msanii huyo.

 

TAARIFA ZA NDANI…

Taarifa kutoka ndani ya familia ya Diamond au Mondi zimeeleza kuwa, kwa siku za hivi karibuni, Tiffah amekuwa akikaririshwa maneno na mama yake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ aseme maneno ambayo yanaweza kumfanya baadaye aje kuichukia familia ya baba yake.

“Unajua Zari ameshaonesha wazi kwamba hataki wanaye wakutane sana na Mondi, mara kadhaa hata Mondi mwenyewe ameshawahi kulisema hilo hadharani sasa matokeo. Anapofanya hivyo maana yake ni kwamba Tiffah na Nillan watakosa nafasi nzuri ya kukaa na baba yao.

 

“Hii ndio changamoto kubwa ya familia zetu za Kiafrika na anapokuwa nao yeye tu muda mwingi watoto ni rahisi sana kumuona baba yao kama vile hawapendi au kupandikiziwa chuki ambayo itawafanya waanze kumchukia baba yao,” kilieleza chanzo hicho.  

FAMILIA YAWEKWA PABAYA

Chanzo hicho kiliweka wazi kuwa, vitendo hivyo vimeiweka familia ya Mondi pabaya kwani wanayaona yale yaliyotokea kwa Diamond na baba yake Mzee Abdul Juma yanaweza kujitokeza kwa Diamond na wanaye kwani watapoteza tu mapenzi na baba yao.

 

“Kuwaweka watoto mbali na baba yao halafu ukionekana unawamezesha maneno yenye viashiria vya kumzungumza baba yao vibaya inaleta picha mbaya. Familia inaliona tatizo ambalo lisipodhibitiwa mapema, litakuja kuwa tatizo kubwa sana huko mbeleni,” kilisema chanzo hicho.

MFANO WAANIKWA

Chanzo hicho kilieleza kuwa, mfano hai ni video ambayo imevuja hivi karibuni katika mtandao wa kijamii wa Instagram ikimuonesha Tiffah akizungumza maneno ambayo familia imeyaona kama ni madongo wanapigwa wao.

 

“Wewe angalia kile kipande cha video utasikia kwa mbali kama vile sauti ya mama Tiffah ikimuelekeza aseme hayo maneno ambapo Tiffah anasikika akisema; mumy is happy, Dady is sad akiwa ana maana kuwa mama yake ana furaha wakati baba yake hana,” kilisema chanzo hicho.

 

NI KWELI DIAMOND HANA FURAHA

Duru za habari za kimastaa zinaonesha kuwa, Diamond hateseki kwa namna yoyote kwa kitendo cha yeye kutengana na Zari ambapo hivi karibuni alitamka hadharani kuwa hakuwahi kumpenda mrembo huyo wa Kiganda kama yeye alivyokuwa yeye akimpenda.

BABA MONDI ANENA

Risasi Mchanganyiko lilimtafuta baba Diamond, na kumuuliza kuhusu suala hilo ambapo kwanza alikiri kulifahamu na kwamba linawaweka kwenye wakati mgumu kama familia. “Unajua mimi kama mzazi naliona hili ni tatizo ambalo endapo Zari hataelezwa na kuacha linaweza kuleta tatizo siku za usoni. Akianza kuwalisha watoto maneno ambayo yana viashiria hasi kwa baba yake, italeta shida tu huko baadaye.

 

“Zari hatakiwi kufanya hivi nilivyosikia anafanya ni hatari sana kwa maisha ya watoto. Nimshauri tu, atafakari kwa kina, ajue kabisa kutengana kwake yeye na Diamond kusilete madhara kwa watoto. Ahakikishe watoto wanampenda baba yao, wanaonana naye na ikiwezekana kuwasiliana mara kwa mara,” alisema baba Diamond.

 

ESMA ANASEMAJE?

Baada ya kumkosa Diamond hewani, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta dada wa msanii huyo, Esma Khan ambapo alipoulizwa kuhusu sakata hilo na kama amekiona kipande cha video kinachomuonesha Tiffah akitupa madongo alisema hawezi kuzungumzia sababu yupo bize na shughuli zake. “Sipo kwenye nafasi nzuri ya kulizungumzia hilo, nipo bize na kazi kwa sasa,” alisema Esma.

 

TUJIKUMBUSHE

Diamond na Zari waliachana Februari 14, mwaka jana baada ya kudumu kwenye uhusiano kwa muda mrefu. Toka hapo, wawili hao wamekuwa na mawasiliano hafifu huku Diamond akiwa wa kwanza kumtangaza mpenzi wake mpya, Zari naye akafuatia baadaye


Loading...

Toa comment