The House of Favourite Newspapers

TIGO FIESTA 2018- VIBE KAMA LOTE YAJA NA PROMOSHENI YA DATA KAMA LOTE

Mkuu wa Huduma na Bidhaa wa Tigo, David Umoh (kulia) akizungumza na waandishi wa Habari leo  katika uzinduzi wa promosheni ya Data Kama Lote inayowapa wateja bonasi ya hadi mara mbili kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya Tigo *147*00#.
Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga  (kulia) akizungumza na waandishi wa Habari leo  katika uzinduzi wa promosheni hiyo.

 

 

 

KAMPUNI inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali, Tigo Tanzania leo imetangaza promosheni murwa kwa wateja wote watakaonunua vifurushi vya intaneti kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00#. Mteja atapokea bonasi la uhakika papo kwa hapo lenye thamani hadi mara mbili ya kifurushi cha intaneti atakachonunua katika msimu huu wa Tigo Fiesta 2018.

 

Akitangaza promosheni hiyo jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh alisema, “Kuendana na msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote, promosheni hii ya Data Kama Lote itahakikisha kuwa wateja wote wa Tigo wanafurahia maisha ya kipekee ya kidigitali huku wakisambaza matukio ya Tigo Fiesta 2018 mubashara kutoka sehemu yoyote ile ya nchi kupitia mtandao wenye kasi ya juu zaidi wa 4G+.”

 

 

Hali kadhalika, Tigo inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Katika mikoa yote ya Tigo Fiesta 2018, wateja wanapaswa kupiga *150*01#  na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika cha bei ya tiketi kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.

 

 

Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya  http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.

 

 

Tigo ni mtandao unaojulikana kwa promosheni kabambe na ubunifu wa kipekee unaoendana na mahitaji halisi ya soko, hivyo kuifanya Tigo kuwa mtandao unaowaelewa wateja wake zaidi.

 

 

Kwa hiyo tumejizatiti kuwapa wateja wetu promosheni bora zaidi katika msimu huu wa Tigo Fiesta 2018. Tunawakaribisha wateja wetu kufurahia ofa hizi murwa.

 

Kuhusu Tigo Tanzania 

Tigo Tanzania ni kampuni ya simu yenye maisha ya kidigitali inayoongoza Tanzania. Tigo ilianza kuendesha shughuli zake nchini Tanzania mwaka 1995.   Kupitia bidhaa zake mbalimbali za kipekee kwenye sauti, ujumbe mfupi, internet yenye kasi na huduma za kifedha kwenye mitandao ya simu za mikononi , Tigo imekuwa mwanzilishi katika ubunifu wa kidigitali kama vile simu ya kwanza ya smartphone kwa kiswahili, Huduma ya facebook kwenye lugha ya kiswahili,  bure, huduma ya TigoPesa, Huduma ya simu ya Tigo pamoja na huduma ya kwanza Afrika Mashariki ya kutuma fedha kwa njia ya simu za mikononi nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili sarafu ya nchi husika.

 

Kwa taarifa zaidi: [email protected]

 

Comments are closed.