Tigo Tanzania Yaendelea Kuunganisha Maeneo ya Vijijini

 Mkurugenzi Mtendaji wa TIGO, Bw. Simon Karikari, akisaini mkataba utakaowezesha kusambaza Mawasiliano kwa wote hususani vijijini, kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga.

Tangu mwaka 2013 Tigo kushirikiana na Serikali kupitia Mfuko wa mawasiliano kwa wote, Tumeweza kupeleka mawasiliano ya simu kwenye vijiji  mbalimbali nchini Tanzania ambavyo siyo Rafiki kwa uwekezaji. Kwa kufanya hivi Tigo inaamini kabisa tutapunguza pengo la mawasiliano kati ya miji na vijijini na pia tutakuza maendeleo ya jamii kwa ujumla.

Kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF), Serikali imeweza kutoa ruzuku na kuwawezesha makampuni ya simu kuweza kuwa na uwekezaji wenye manufaa kwa wananchi kwa ujumla.Mpaka sasa Tigo imeweza kujenga minara 169 kwenye vijiji 116.

Mwaka huu tuna mpango wa kufikia vijiji vingine 13. TIGO imewekeza shilingo billioni 17.1 na inategemea kuwekeza bilioni 1.8 zaidi. Kupitia kwa mradi huu, TIGO tumeweza kuwafikia watu wengi Zaidi na tunaamini kabisa kupitia mawasiliano, tumebadilisha namna ambavyo watu wanafanya biashara, wanaelimika, wanafanya kilimo na hata ufanyaji wa kazi zao mbalimbali za kila siku.

Tunaamini kabisa kwa kupeleka mawasiliano tunachochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na jamii nzima kwa ujumla.


Loading...

Toa comment