The House of Favourite Newspapers

Tigo Yawakabidhi Mamilioni Na Vifaa Vya Hisense Washindi wa Droo ya Saba Kampeni Ya Ndinga la Kishua

0
Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Rutta (kushoto) akimuonesha mmoja wa washindi vifaa vyake wakati akimkabidhi.

Dar es Salaam, 13 Januari 2023: Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo inayoendesha kampeni ya Ndinga la Kishua Mamilioni ya Pesa na vifaa vya Hisense imewakabidhi zawadi zao washindi wa droo ya saba ya kampeni hiyo.

Katika droo hiyo washindi wanne walikabidhiwa pesa taslimu shilingi milioni moja kila mmoja na washindi wawili kila mmoja alikabidhiwa vifaa vya Hisense ambavyo ni Tv ya kisasa smart 4k inchi 50, friji, microwave na spika za muziki za kisasa ‘sound bar’

Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Rutta (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi mmoja wa washindi wa shilingi milioni moja.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi zawadi hizo Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Rutta amesema washindi hao wamepatikana kutokana na kutumia huduma za Tigo Pesa.

Mary Rutta aliendelea kusema wakati akikabidhi zawadi hizo;

“Tupo kwenye tukio la kutoa zawadi kwa washindi wetu wa droo ya saba na tumebakiza wiki moja kumaliza kampeni hii na pia tumebakiza droo kubwa ya kushinda milioni kumi na milioni ishirini pamoja na gari aina ya Toyota Rush jipya kabisa ziro kilomita”.

Washindi wa shilingi milioni moja wakiwa na mfano wa hundi ya pesa walizojishindia.

“Hivyo basi napenda kuwasisitiza watumiaji wa simu za mkononi kufanya kutumia huduma za mtandao wa Tigo na kutumia huduma za Tigo Pesa kufanya miamala mbalimbali ili waingie kwenye droo hii na kuweza kuwa washindi.

“Miamala hiyo ni kama vile kulipa bili, kutuma na kupokea pesa, kupokea na kutuma pesa kutoka benki au mitandao mingine au nchi za nje pamoja na kufanya malipo ya serikali chukua mikopo kutoka huduma yetu ya Nivushe na Bustisha ili ujiongezee nafasi ya kuwa mshindi”.

Mmoja wa washindi wa vifaa vya Hisense, Mariam Kuna akisimamia vifaa vyake alivyojishindia wakati vikipakiwa kwenye gari lake aondoke navyo.

Kwa upande wake Afisa Masoko wa Kampuni ya Hisense, Joseph Mavula akizungumza kwenye tukio hilo alisema;

“Siku ya leo tunakabidhi washindi wetu wa kampeni ya Ndinga Kishua, Mamilioni ya Pesa na Vifaa vya Hisense ambapo tuna washindi waliojishindia pesa taslimu pia tuna washindi wawili waliojishindia vifaa vya Hisense ambavyo ni Tv ya inchi 50 ya kisasa kabisa smart 4k, friji, microwave na spika za muziki wa kisasa (sound bar)

“Tunawasisitiza zaidi kuendelea kufanya miamala ya Tigo Pesa ili kuendelea kujishindia.

“Wiki hii tumepata washindi wawili wa vifaa vya Hisense na wiki ijayo tunatarajia kupata washindi wengine wawili ambao watakuwa wa mwisho.

“Lakini pia Kampuni yetu ya Hisense inaendelea kutoa punguzo la asilimia kwenye maduka yetu yote yaliyoidhinishwa hapa nchini ukinunua kwa huduma ya Lipa kwa simu”. Alimaliza kusema afisa huyo.

Leave A Reply