The House of Favourite Newspapers

Tigo Yampata Mshindi Wa Ndinga La Kishua, Wengine Waibuka na Mamilioni

0
Mwanamitindo, Hamisa Mobetto na Mwanahabari Millard Ayo (katikati) wakichezesha droo hiyo, kushoto ni Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Rutta na kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Rasul Masoud akihakikisha washindi wanapatikana kwa haki.

Dar es Salaam 19 Januari 2023: Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo hatimaye jana imempata mshindi wa Ndinga la Kishua aina ya Toyota Rush mpya kabisa ‘ziro kilomita’ kwenye droo ya mwisho ya Kampeni ya Ndinga la Kishua Mamilioni ya Pesa na Vifaa vya Hisense ambaye ni Bwana Samson kutokea Kahama mkoani Shinyanga.

Droo hiyo ilichezeshwa hadharani na wahamasishaji wa kampeni hiyo, mwanamitindo, Hamisa Mobetto na mwanahabari Millard Ayo wakiongozwa na Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Rutta na kusimamiwa na Afisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Rasul Masoud.

Mwanahabari Millard Ayo akimpigia simu mshindi wa Ndinga la Kishua baada ya namba yake kuibuka na ushindi.

Sambamba na ushindi wa Samsom ambaye ni mfanyakazi kwenye bekari ya kuoka mikate wengine waliomsindikiza kwenye ushindi wake ni James Gabriel anayefanya shughuli zake Mlimani City Dar ambaye namba yake iliibuka na ushindi wa milioni 10 pamoja na Bi Mary mkazi wa Chanika, Dar aliyejishindia milioni 20.

Kwa washindi hao ilikuwa ni siku ya vifijo na nderemo kwa kila aliyepigiwa simu kupewa taarifa za ushindi wake huku wengine wakionekana kupigwa butwaa na kutoamini walipopigiwa simu mpaka walipothitishiwa kuwa namba iliyotumika kuwapigia ni namba 100 ambayo haiwezi kutumiwa na matapeli ndipo vifijo na nderemo zao zilizidi kuongezeka.

Kama zilivyokuwa droo zilizopita washindi wengine namba zao ziliibuka kwenye droo ya ushindi wa vifaa vya Hisense na milioni mojamoja.

Droo hiyo iliyokuwa ya nane na ya mwisho ambapo washindi hao waliibuka kwa kufanya miamala ya Tigo Pesa kama kwa wingi kama vile kulipa bili, kutuma na kupokea pesa, kupokea na kutuma pesa kutoka benki au mitandao mingine au nchi za nje pamoja na kufanya malipo ya serikali chukua mikopo kutoka huduma yetu ya Nivushe na Bustisha. Alisema Mary Rutta.

Leave A Reply