The House of Favourite Newspapers

Tigo Yawapeleka Dubai Kuinjoi Washindi 16 Wa Magifti Dabodabo Awamu Ya Kwanza

0
Washindi wa Safari ya Dubai a.k.a Dubenga na wapendwa wao wakiwa kwenye picha ya pamoja Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kupaa kuelekea nchini humo kuinjoi.

Dar es Salaam, 12 Desemba 2023: Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo imewapeleka Dubai washindi 16 wa kampeni yake ya Magifti Dabodabo awamu ya kwanza ambapo hao walijishindia safari hiyo kwa kutumia huduma za kampuni hiyo kununua vocha, kuongeza salio kwa Tigo Pesa, kufanya miamala mbalimbali kama vile kulipa bili, kununua umeme, maji, kutumia huduma za lipa namba na nyinginezo.

Semaji la Kampeni ya Magifti Dabodabo, Haji Manara katikati (mwenye mtoto) akiwa na washindi na wapendwa wao muda mfupi kabla ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kupaa kuelekea ‘Dubenga’.

Akizungumza kwenye hafla ya kuwaaga washindi hao zilizofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Rutta amesema safari hiyo ni awamu ya kwanza na kuwataka watumiaji wengine wa simu za mkononi kutumia mtandao wa Tigo ili waweze kuibuka na ushindi katika awamu zinazofuata kwakuwa kampeni hii bado inaendelea mpaka mapema mwakani.

Meneja huyo amesema kama inavyoitwa kampeni hiyo Magifti Dabodabo unaposhinda zawadi unamtafuta wa kushinda nae hiyo hata hao wa safari ya Dubai nao wameungana na wapendwa wao katika safari ambayo watainjoi kwa siku tano wakiwa wameshalipiwa kila kitu.

Pamoja na ushindi wa safari hiyo zawadi zingine ambazo zinaendelea ni safari hiyo kwa awamu zingine, safari ya Zanzibar, pesa taslimu shilingi milioni moja, milioni tano, milioni kumi, seti ya vifaa vya umeme vya ndani ambavyo ni runinga za kisasa, seti ya muziki ya kisasa (Sound Bar) friji na oven pia kuna gari za kisasa ambapo zawadi hizo nazo zitatolewa dabodabo kwa atakayeibuka mshindi na mpendwa wake.

Leave A Reply