The House of Favourite Newspapers

TIMU TATU BORA RBA ZILIVYOJIPANGA MSIMU MPYA

MSIMU mpya wa Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (RBA), unatarajiwa kuanza Februari, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar.

 

Jumla ya timu 16 zikiwemo za wanaume na wanawake, zinatarajiwa kuvaana ipasavyo katika ligi hiyo, yenye kufuatiliwa na mashabiki lukuki wenye staili tofauti za ushangiliaji.

 

Tujikumbushe kidogo; msimu uliopita kwenye Ligi ya RBA, timu ya Savio ilifanikiwa kuwa bingwa baada ya kuifunga Oilers pointi 56-51 katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar.

 

Kabla ya fainali hiyo kuchezwa, Septemba 23, mwaka jana, mchezo wa nusu fainali ulishuhudiwa ukizipambanisha timu za jeshi, ABC na JKT, katika mchezo huo, JKT hawakutokea uwanjani, ABC wakapewa ushindi wa mezani.

Wakati tukielekea kwenye msimu mpya wa RBA, tayari Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD), kimetangaza kuanza maandalizi ya msimu huo wa 2019, ikiwa ni pamoja na kusaka wadhamini sambamba na uwepo wa mabadiliko yenye tija kwa klabu zote shiriki.

 

Tukiachana na BD, timu mbalimbali nazo zina morali ya hali ya juu kuelekea msimu huo, wachezaji nao kama kawaida kujitapa hawaachi, wengi wamepania kufanya makubwa na kila mmoja anataka kuweka heshima katika klabu yake.

 

Zifuatazo ni timu tatu zilizoshika nafasi za juu kwenye Ligi ya RBA msimu uliopita ambapo viongozi wa klabu hizo na wachezaji pia, wamezungumza na Championi Jumatano kila mmoja kumzungumzia mwenzake katika safari ya kuwania ubingwa wa mwaka huu.

SAVIO

Kwa mara ya nne mfululizo, timu ya Savio imeshikilia ubingwa wa RBA, na kuziacha timu mbalimbali zikigombea nafasi zilizobaki. Huyu hapa msemaji wa Savio, Abdul Mntaimbo, anadadavua mambo mbalimbali kuhusu na namna walivyojiandaa kuutetea ubingwa w a o m s i m u huu.

 

“Kuanzia mwaka 2015 h a d i 2 0 1 8 , tumeend e l e a kushikilia ubingwa wa RBA, lakini pia miaka ya n y u m a tuliwahi k u w a m a b ingwa wa ligi hiyo zaidi ya mara nne.

 

“Kuelekea msimu huu, tumeanza maandalizi kabambe yatakayoleta mapinduzi kwa timu pinzani, tutafanya usajili wa wachezaji watano wa kigeni sambamba na kuwapandisha wawili kutoka timu yetu ndogo ya Young Stars. “Wapinzani wetu nawashauri wasiufikirie hata kidogo huu ubingwa kwa sababu maandalizi tunayoendelea nayo si mchezo, mwaka huu tutazionyesha timu pinzani sisi ni nani,” anasema Mntaimbo.

 

OILERS

Lusekelo Mbwele, ndiye kocha mkuu wa timu hii iliyokamata nafasi ya pili msimu uliopita wa RBA. Kumaliza ligi hiyo wakiwa nafasi ya pili haikuwa akilini mwao, kilichotokea ni kuzidiwa nguvu na wapinzani wao Savio huku wakikiri kuwa, hilo halitajirudia tena msimu huu.

 

Huyu hapa Mbwele anasema: “Msimu huu Savio watakiona cha moto, kama mwaka jana walitufunga fainali basi mwaka huu tutawatembezea kichapo kuanzia mechi ya kwanza hadi ya mwisho na kuhakikisha tunaweka historia kwa mara ya kwanza kuwa mabingwa wa ligi hiyo.

 

“Oilers tumeshaanza mazoezi kuelekea msimu mpya wa RBA ninaoutabiri kuwa na ushindani mkubwa dhidi ya timu zote zitakazoshiriki.

 

“Kwa upande wa kikosi changu, sina sababu ya kusajili wachezaji wapya kwa sababu hawa nilionao wananitosha, viwango vyao ni vikubwa mno na naamini vitaleta changamoto kwa wapinzani hatimaye kuibuka mabingwa.”

 

ABC Tayari timu ya ABC yenye wachezaji wakongwe wa mpira wa kikapu, wanaendelea na mazoezi ya kila siku kwenye uwanja wao wa 95 uliopo pembezoni mwa Uwanja wa Taifa jijini Dar.

 

Salim Mchemba ambaye ni staa wa kikosi hicho, anathibitisha kuanza mazoezi ya kila siku kujiandaa na mashindano mbalimbali ikiwemo Ligi ya RBA. “Mazoezi yanaendelea kila siku asubuhi kwenye Uwanja wetu wa 95, wachezaji tupo vizuri, tunajituma kama kawaida yetu.

 

“Nikizungumzia msimu uliopita, ushindani ulikuwa mkubwa sana, mwaka huu natabiri hilo kwani kila timu itajipanga kuchukua ubingwa lakini tunaahidi mashabiki wetu kucheza kwa kujituma ili tuchukue ubingwa,” anasema Mchemba.

Makala: Sharifa Mmasi, Dar es Salaam

Comments are closed.