The House of Favourite Newspapers

TMA: Kimbunga Jobo Kimepungua Nguvu

0

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema Kimbunga Jobo kilichokuwa kinatarajiwa kupiga Pwani ya Tanzania kwa siku mbili, leo April 24 na kesho, April 25, kimepungua nguvu kwa haraka baada ya kuingia katika mazingira yenye mzunguko wa upepo kinzani hivyo kwa sasa ni kimbunga hafifu kinachosafiri kwa kasi ya kilometa 18 kwa saa baharini.

Katika taarifa huishwa iliyotolewa na mamlaka hiyo leo, kimbunga hicho kwa sasa kipo umbali wa kilometa 200 Mashariki mwa Kisiwa cha Mafia na kupungua kwake nguvu kunatarajiwa kusababisha vipindi vya mvua kubwa katika maeneo machache ya ukanda wa Pwani kati ya leo na kesho, huku pia kikisababisha mawimbi makubwa baharini.

 

Maeneo yanayotarajiwa kupata athari za moja kwa moja kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa, ni pamoja na mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani ikiwemo Kisiwa cha Mafia, Dar es Salaam na kisiwa cha Unguja.

Leave A Reply