The House of Favourite Newspapers

TMSA Kutoa Tuzo Bora za Masoko Tanzania za Mwaka 2022

0
Mwenyekiti wa Bodi ya TMSA, Dkt. Emmanuel Chao (PhD) (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la ugawaji tuzo za masoko kwenye vipengele 14. Tukio hilo litafanyika Ijumaa Julai 22 mwaka huu katika Jengo la PSSSF. Mwanzoni kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Josephine Msalilwa kutoka Coca-Cola ambao ni miongoni mwa wadhamini wakuu wa tuzo hizo.

 

Dar es Salaam, 20 Julai. Katika nia ya kuhamasisha weledi zaidi katika sekta ya masoko nchini Tanzania, Chama cha Sayansi ya Masoko Tanzania (TMSA) kinatarajiwa kutoa tuzo katika vipengele 14 tofauti vya masoko kwa mwaka 2022.

 

Tuzo hizi za masoko 2022 zitafanyika Julai 22 jijini Dar es Salaam, na tuzo hizi zimevutia kampuni kubwa kudhamini na kushiriki kwenye tukio hili. Tangu mwaka wa 2021, TMSA imetumia tuzo hizo ili kuakisi juhudi na mafanikio ya watu binafsi, mashirika, na wasomi ambao wanaleta mabadiliko katika Nyanja ya masoko.

 

Akizungumza na vyombo vya habari, Mwenyekiti wa Bodi ya TMSA, Dkt. Emmanuel Chao (PhD), alieleza jinsi masoko kuwa nguzo muhimu ili kuhakikisha ukuaji wa kampuni na kuleta faida. Alisema, “Katika biashara yoyote, idara ya masoko ni ya kipekee, kwani inajumuisha kati ya asilimia 30 na 40 ya bajeti ya biashara, na ndio kati ya msingi wa kudumisha biashara yoyote”.

 

Aliendelea, ‘kwahiyo, kama TMSA, tutatumia fursa hii kuhimiza makampuni na watendaji kuwa na weledi zaidi katika hii idara. Na kwa bahati nzuri, katika TMSA, tayari tunatoa programu za masoko. Pia tuko kwenye mazungumzo na Taasisi ya Chartered Marketing Institute ya nchini Uingereza UK kushirikiana kwenye uandaaji wa programu mbalimbali za masoko.

 

Nia yetu ni kuhakikisha soko la ndani linafaidika zaidi kwa kuzalisha wataalamu waliohitimu na wenye uelewa zaidi wa soko la Afrika kuliko soko la nje’’.

 

Mmoja wa wadhamini wakuu, kampuni ya Coca-Cola ambayo iliwakilishwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Josephine Msalilwa alikiri kuwa tuzo hizo zitakuwa chachu katika kuchochea ukuaji wa sekta ya masoko. Alinukuliwa, “Tuko pamoja na TMSA katika utoaji watu zo za TMSA, na tuna matumaini yetu ni kuwa huu ni mwelekeo sahihi wa kuhamasisha ubunifu na weledi miongoni mwa wafanyabiashara wa Tanzania,” alisema.

 

Mchakato wa kuchagua na kuteua washindi wa tuzo uliendeshwa mtandaoni, ambapo watu binafsi na mashirika yaliteuliwa. Baada ya mchakato wa uteuzi huo, timu ya majaji wenye uzoefu ilipitia uteuzi uliopendekezwa na washindi waliochaguliwa.

Leave A Reply